Bilionea namba moja Duniani Elon Musk
BILIONEA namba moja Duniani Elon Musk ametoa ofa ya Dola Bilioni 43.4 kununua mtandao wa kijamii wa Twitter.
Kwa mujibu wa CNN Business inadai Musk ametuma ofa hiyo ili kumiliki hisa ambazo hazimiliki kwa sasa zenye thamani ya kiasi cha dola 54.20 kwa kila hisa.
Elon Musk ametuma ofa ya Dola Bilioni 43.4 kuinunua Twitter
Musk amesema kiasi hicho cha ofa aliyotoa ndiyo ofa bora na ya mwisho kutoka kwake na kwa mujibu wa SEC ni kwamba Musk alidai ofa hiyo isipokubaliwa basi ataangalia upya nafasi yake kama mwekezaji kwenye Kampuni hiyo.
Twitter ipo njiani kununuliwa na Elon Musk
Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Tesla alinukuliwa akisema:
“Naamini kwamba Kampuni inabidi imilikiwe ili kuweza kupitia mabadiliko mbalimbali ambayo yanatakiwa yafanyike.”
Social Plugin