DKT. GWAJIMA AKAGUA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA MANISPAA YA SHINYANGA...AIPA TANO AGAPE KUJENGA SHULE YA WAATHIRIKA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akikagua ujenzi ya shule ya Sekondari ya wasichana Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, ametembelea shule ya Sekondari Agape iliyopo Chibe Manispaa ya Shinyanga, ambayo inasomesha madhura wa matukio ya ukatili, pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.


Waziri Gwajima amefanya ziara hiyo leo, Aprili 24,2022 akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi, Maofisa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, viongozi wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.


Akizungumza katika shule ya Agape, Dkt. Gwajima amepongeza kuanzishwa shule hiyo, ambayo inatimiza ndoto za wanafunzi zilitoka kuzimwa kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili, ikiwamo kupewa mimba na kuozeshwa ndoa za utotoni na kukatishwa masomo yao.

Amesema Shirika la Agape limefanya kazi kubwa ya kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili na hata kusaidia madhura wa matukio hayo kutimiza ndoto zao, huku akiahidi Serikali kuendelea kuwaunga pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.

“Serikali tunalipongeza Shirika la Agape kwa kusaidia kutimiza ndoto za madhula hawa wa ukatili, sababu bila nyie huenda wagekuwa na maisha magumu na wengine kuishi mitaani wakilanda, lakini mmefanya kazi kubwa ya kuwaokoa na sasa wanasoma na kutimiza ndoto zao,”
amesema Dkt. Gwajima.

“Nimefurahi kusikia taarifa ya watoto hawa kuwa Tisa wamemaliza elimu ya chuo kikuu na wapo kwenye ajira tayari na 22 bado wapo vyuoni, na wengine wakiendelea na masomo ya kidato cha Sita, Tano na vidato vingine jambo ambalo linahitaji pongeza na watoto hawa watakuja kuwa viongozi wa taifa hili baadae,”anaongeza Gwajima.

Aidha, ametoa wito kwa watoto hao fursa ambayo wameipata ya kusoma, wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao, huku akiitaka jamii iache kuwafanyia vitendo vya ukatili watoto wa kike bali wawache wasome na kutimiza malengo yao.

Katika hatua nyingine Waziri Gwajima, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha Sh. bilioni 4.5 na kutanguliza bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Manispaa ya Shinyanga, ambayo itasaidia kutimiza ndoto za wanafunzi na kuepukana na changamoto ya vishawishi njiani sababu watakuwa wakikaa bweni.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amesema wanachokifanya Agape ni ibada na Mungu atawalipa kwa kitendo ambacho wanakifanya cha kuokoa ndoto za wanafunzi wa madhula wa mimba na ndoa za utotoni, huku akiahidi Serikali kuendelea kuwaunga mkono.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, ameishukuru Serikali kwa kuwasaidia hasa pale wanapopitia kwenye kipindi kigumu ikiwamo upungufu wa chakula kwa ajili ya kulisha watoto hao, pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali ikiwamo kadi za bima za Afya.

Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima, akizungumza katika Shule ya Sekondari Agape.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza katika Shule ya Sekondari Agape.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akizungumza katika Ugeni wa Waziri Gwajima katika shule yao ya Sekondari.

Meneja wa Shirika la Agape Peter Amani akisoma taarifa ya Shule ya Sekondari Agape.

Muonekano wa jengo katika Shule ya Sekondari Agape.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, akizungumza katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Manispaa ya Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, akizungumza kwenye ujenzi wa shule hiyo ya wasichana Manispaa ya Shinyanga.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye ujenzi wa shule hiyo ya wasichana Manispaa ya Shinyanga.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akikagua ujenzi ya shule ya Sekondari ya wasichana Manispaa ya Shinyanga.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akikagua ujenzi ya shule ya Sekondari ya wasichana Manispaa ya Shinyanga.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, akikagua ujenzi ya shule ya Sekondari ya wasichana

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa majengo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Manispaa ya Shinyanga.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima wa pili (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) na kikundi cha wanawake ambacho kimepewa mkopo na Halmashauri wakiwa katika Shamba la Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post