Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO, RAS ATAKA WAWE WAAMINIFU, WAAJIRI WATENDAJI WENYE SIFA

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Aprili 28,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mjini Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imewataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kuwa waaminifu katika kulipa wakulima bei stahiki na kujitahidi kudhibiti ubora wa mazao, usafi wa mazao na vipimo sahihi wakati wa kuuza mazao ili yaweze kupata bei nzuri.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Aprili 28,2022 na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika (Madini, pamba na tumbaku) mkoa wa Shinyanga yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya usimamizi wa Ushirika, kujiendesha kibiashara na Maadili ili waweze kufanya shughuli zao vizuri.

Omary ameshauri pia mazao yaliyopo kwenye Ushirika ambayo ni Pamba, Korosho,Mkonge na Tumbaku yapangwe katika madaraja sahihi ili kumrahisishia mnunuzi kutoa bei nzuri zaidi kuliko kuchanganya.

“Hivi sasa tunaelekea msimu wa masoko kwa mazao ya pamba na tumbaku. Niwaombe tujaribu kusimamia masoko yetu vizuri ili kuhakikisha changamoto za msimu uliopita hazijirudii.Tuweke mifumo mizuri ya uuzaji za ulipwaji wa pesa zetu hasa upande wa vyama vya pamba,tuachane na malipo ya pesa taslimu yatatuchelewesha maendeleo na kutusababishia migogoro ya upotevu na wizi wa pesa za pamba”,amesema Omary.

“Pia tuimarishe zaidi usimamizi wa vyama vya ushirika kwa kuajiri watendaji wenye sifa badala ya kuleana na kubebana. Hili naomba sana Mrajis Msaidizi wahimize Maafisa Ushirika wako wavielekeze vyama kuajiri watendaji wenye sifa ambao wana uwezo wa kutuvusha na kutufikisha mahali tunapopatarajia kufika la sivyo vyama hivi havitabadilika”,ameongeza.

Amebainisha kuwa serikali inahitaji kuona vyama vya ushirika vikijiendesha na kusimamiwa vizuri kwa misingi ya Ushirika badala ya kufanya mambo kwa mazoea.

Aidha amewahimiza wana ushirika kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kufanya kazi kwa bidii na kulima kilimo chenye tija na kilimo cha kisasa kuachana na kilimo cha mazoea kwani serikali inaendelea kutoa fursa mbalimbali za kumkomboa mkulima ikiwemo kutoa dawa na mbegu bure,kuboresha huduma za ugani kwa kugawa vitendea kazi kwa maafisa ugani nchi nzima na benki kupunguza riba kwenye kilimo.

Katika hatua nyingine amevitaka Vyama vya Ushirika kuhakikisha vinachagua viongozi wenye uwezo kwa kufanya kazi kwa misingi ya utawala bora badala ya kufanya kazi kwa mazoea huku akisisitiza kuwa viongozi hao wanatakiwa kuwa wenye maono,wabunifu na kuwea kuzitunza na kuzilinda mali za wana ushirika na siyo kuhujumu mali hizo.

“Kwa sasa mkoa wa Shinyanga una jumla ya maafisa ushirika 7 katika halmashauri sita lakini Ofisi ya Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa anayesimamia vyama 452 vya mkoa mzima hana hata afisa ushirika wa kumsaidia kakzi kwenye ofisi yake. Suala hili serikali kupitia Wizara ya Kilimo inaendelea kulitafutia ufumbuzi ili kuwa na idadi ya watumishi wanaotakiwa”,amesema.

“Jukumu la kuubadilisha ushirika wetu siyo la mtu mmoja ni letu sote. Jukumu hili siyo la Mrajis Msaidizi mkoa pekee lazima tusaidiane naye kuhakikisha mipango iliyowekwa na Tume ya maendeleo ya Ushirika pamoja na maono ya wana ushirika tunasaidiana kuyatekeleza kwa pamoja na kwa umoja wetu. Na huo ndiyo ushirika wenyewe na hiyo ndiyo dhana ya ushirika”,ameongeza Omary.

Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace amesema mafunzo hayo kwa Wajumbe wa bodi yanatarajiwa kuleta tija kwa kuonesha mabadiliko chanya kwa viongozi wa vyama vya ushirika katika maeneo wanayoyasimamia.

“Mafunzo haya yana lengo la kukumbushana wajibu na mipaka ya vyama vya ushirika,kubadilishana mawazo,kuwakutanisha na wadau wa sekta ya kilimo ili kuonesha fursa zilizopo kwani tunataka vyama vya ushirika vinakuwa endelevu”,amesema Boniphace.

“Tunataka Ushirika uwe imara na ujiendeshe kibiashara. Tunashukuru viongozi wa vyama vya ushirika wamehudhuria mafunzo haya kwa wingi tofauti na matarajio yetu hii inaonesha ni kiasi gani wanataka mabadiliko katika kuboresha utendaji kazi wao”,amesema.

Mkoa wa Shinyanga una jumla ya vyama vya Ushirika vya Msingi 457 vyenye jumla ya wana ushirika 46,395. Pia kuna vyama vya Upili vitatu vinavyojumuisha Union mbili za SHIRECU LTD na KACU LTD vyenye jumla ya vyama wanachama na mkoa una jumla ya SACCOS 7 tu ambazo zimepata leseni kati ya SACCOS 20 zilizokuwepo hapo awali.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Aprili 28,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Aprili 28,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mjini Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Aprili 28,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mjini Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Aprili 28,2022 katika ukumbi wa SHIRECU Mjini Shinyanga.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace akizungumza kwenye mafunzo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga

Mwezeshaji Charles Malunde akitoa mada kwenye mafunzo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga
Mwezeshaji Charles Malunde akitoa mada kwenye mafunzo kwa Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga
Viongozi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com