Tukio la kusikitisha limetokea katika Kanisa la Evangelical Winning All (ECWA) nchini Nigeria baada ya shemasi kuanguka ghafla na kufariki papo hapo akihubiri dhidi ya mauaji ya kiibada na dhabihu za kibinadamu.
Imeibuka kuwa kisa hicho kilitokea Jumapili, Aprili 3,2022 wakati shemasi huyo aliyetambulika kwa jina moja la Ogunnusi, alipokuwa akihubiri wakati wa ibada.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Ogunnusi anaonyeshwa akihubiri kwa lugha ya Kiyoruba na ananukuliwa akisema: “Fedha unazopata kwa njia zisizo halali, kuua watu, kunyonya damu ya binadamu; kifo kikija, kitakuwa cha mtu mwingine.” Mkalimani katika ibada hiyo alikuwa bado anajaribu kutafsiri maneno yake kwa Kiingereza wakati Ogunnusi alipoanguka ghafla.
Kulingana na ripoti ya Daily Trust, shemasi huyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Shirikisho, Idi-Aba, Abeokuta, ambapo alithibitishwa kufariki.
Mmoja wa mashahidi aliyezungumza na chapisho hilo alisema: “Mtu huyo hakuwa mchungaji wa kanisa hilo, alikuwa tu mzee wa kanisa. Alikuwa Baale wa Onikoko. Lakini yeye ndiye aliyetoa mahubiri siku ya Jumapili." “Alikuwa anazungumzia kifo na watu wanaopata pesa kwa kuua watu wengine. Ghafla, alianguka.
Alikimbizwa FMC, lakini alikufa. Hatujui kilichotokea. Niliogopa sana. Kila kitu kilivurugika. Tulishiriki tu ombi la neema na tukarudi nyumbani."
Mauaji ya kiibada yamekuwa yakiongezeka nchini Nigeria katika siku za hivi karibuni.
Katika azma ya kukabiliana na maovu hayo, Serikali ya Shirikisho ilikuwa imefichua mipango ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji dhidi ya mila ya pesa ambayo imegharimu maisha ya wengi, haswa wanawake na wasichana.
Waziri wa Habari na Utamaduni nchini humo Alhaji Lai Mohammed alisema serikali inasikitishwa na kuongezeka kwa visa hivyo kidesturi yanayofanywa na watu wasio waaminifu, wengi wao wakiwa ni vijana wanaotaka kutajirika haraka.
Serikali ya shirikisho pia ilielekeza watengenezaji filamu wa Nigeria kuacha maudhui ya tambiko ya pesa kutoka kwa sinema zao.
Mohammed alisema baadhi ya watu wanaoshukiwa kuwa wauaji wa kitamaduni ambao wamekamatwa walikiri kwamba walijifunza vitendo vya mauaji ya kiibada kwenye mitandao ya kijamii na hii imetaka Serikali ya Shirikisho ibadilishwe ili kusafisha mitandao ya kijamii.