Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi baiskeli Salome Samwel.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu, wamekabidhiwa vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kutoka kampuni ya Barrick, ili kuwaongezea furaha na kuwawezesha kushiriki shughuli za kiuchumi.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa Aprili 7,2022 na Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul, wakati wa hafla fupi iliyohudhuriwa na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mhe. Charles Fussi.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni Baiskeli 30 za kawaida na zile za kusaidia kutembea kwa watu wenye ulemavu, vifaa vya kusikia 5, fimbo nyeupe 6, vyerehani vya kushonea ngozi 2, vyerehani vya kawaida 8 na vya Overlock 2, samani na seti ya Televisheni kwa ajili ya Kituo cha afya Bugarama na pikipiki moja itakayotumika katika ofisi ya Dawati la Jinsia kusaidia kuwezesha kushughulikia masuala ya wasichana na Wanawake.
“Vifaa hivi tulivyokabidhi vina thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40 zikiwa ni kati ya shilingi Bilioni 2.5 zilizotengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa ajili ya miradi ya Uwajibikaji wa Jamii (CSR) kwa mwaka 2021/2022 katika Halmashauri ya Msalala. Dhamira yetu ni kuhakikisha tunatekeleza wajibu wetu katika jamii na kushirikiana nao katika kupanga mipango ya maendeleo hasa inayohusu kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla kupitia mpango wetu wa CSR”,amesema Paul.
“Tunajivunia kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tunajali watu wenye ulemavu wanaoishi maeneo jirani na mgodi wetu ili kuwaongezea furaha na kuwawezesha kushiriki shughuli za kiuchumi kwa kuwapa vifaa vya kazi. Tutaendelea kujivunia kuwajali makundi maalumu kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na dawati la jinsia linaloshughulika na wasichana na Wanawake nao wananufaika”,ameongeza.
Akizungumza wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ameushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya CSR ili kuhakikisha jamii inapiga hatua kimaendeleo.
“Niwapongeze Barrick kwa vifaa hivi mlivyotoa leo kwa kuhakikisha watu wenye mahitaji maalumu wanapata vifaa vitakavyowezesha kufanya kazi. Kwa kweli mmeunga mkono kwa vitendo dhamira na nia ya Mhe. Rais Samia Suluhu, mtetezi namba moja wa watu wenye mahitaji maalumu ambaye mara kwa mara amekuwa akisisitiza makundi maalumu yasiachwe nyuma yapewe kipaumbele katika jamii”,amesema Kiswaga.
Kiswaga amesema Serikali itaendelea kuwajali na kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu katika kupambana na umaskini ili kuhakikisha wanawapa ahueni ya maisha huku akiwashauri watu wenye mahitaji maalumu kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa katika halmashauri za wilaya.
Kiswaga amesema Barrick wamekuwa wakitoa fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali hivyo kuwaagiza watendaji wote kuhakikisha fedha zinatumika kuwaletea maendeleo wananchi na kwamba hatasita kuwashughulika wale wataothubutu kudokoa fedha hizo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Charles Fussi amewataka watu wenye ulemavu kujitokeza kupata mikopo bila riba inayotolewa katika halmashauri huku akishauri kuwa kabla ya kuchukua mikopo ni vyema wakapata ushauri kuhusu miradi inayotekelezeka ili wainuke kiuchumi na kuweza kurudisha mikopo hiyo.
Nao Watu wenye ulemavu akiwemo Salome Samweli na Mshikila Juma ameushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Halmashauri ya Msalala kwa kuwapatia vifaa vya usaidizi ambavyo watavitumia kutembea kutoka eneo moja hadi jingine na kujitafutia kipato ili kujiinua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Watu wenye Ulemavu kata ya Bulyanhulu, Abbas Hassan ameishukuru Serikali na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuwathamini na kuwajali watu wenye ulemavu na kwamba kutokana na vifaa hivyo walivyopatiwa sasa wataweza kuwahi kufika kwenye maeneo yao ya kazi.
Naye mwakilishi wa wazee, Ramadhan Salehe amesema Barrick Bulyanhulu wameonesha upendo kwa kuwapatia bima za afya ambazo zitawawezesha kupunguza gharama za matibabu kwao na wategemezi wao.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu. Wa kwanza kushoto ni Mrakibu wa Mahusiano ya Jamii Barrick Bulyanhulu Bi. Zuwena Senkondo akifuatiwa na Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Charles Fussi. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Charles Fussi akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mrakibu wa Mahusiano ya Jamii Barrick Bulyanhulu Bi. Zuwena Senkondo akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa mbalimbali vya usaidizi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa mbalimbali vya usaidizi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa mbalimbali vya usaidizi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi baiskeli mmoja wa watu wenye ulemavu. Baiskeli hizo zimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Salome Samweli akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa Baiskeli na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga. Baiskeli hizo zimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mshikila Juma akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa Baiskeli na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (aliyeshikilia kipaza sauti kushoto). Baiskeli hizo zimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Cherehani ya Overlock kwa ajili ya kikundi cha wazee. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akikabidhi Cherehani ya Overlock kwa ajili ya kikundi cha wazee. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Cherehani ya Ngozi kwa ajili ya kikundi cha watu wenye ulemavu. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Cherehani ya kawaida kwa ajili ya kikundi cha wazee. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (wa pili kulia) akikabidhi Dish la DSTV ambayo ni sehemu seti ya Televisheni kwa ajili ya Kituo cha afya Bugarama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kulia) akikabidhi TV ambayo ni sehemu seti ya Televisheni kwa ajili ya Kituo cha afya Bugarama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (wa pili kulia) akiwasha pikipiki iliyotolewa na Barrick Bulyanhulu itakayotumika katika ofisi ya Dawati la Jinsia kusaidia kuwezesha kushughulikia masuala ya wasichana na Wanawake.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akiangalia baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Fimbo nyeupe zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Fimbo nyeupe zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akikabidhi Vifaa vya kusikia vilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi kadi za bima ya afya zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Zoezi la kukabidhi kadi za bima ya afya zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu likiendelea.
Zoezi la kukabidhi kadi za bima ya afya zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu likiendelea.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Watu wenye Ulemavu kata ya Bulyanhulu, Abbas Hassan akiishukuru Serikali na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuwathamini na kuwajali watu wenye ulemavu.
Mwakilishi wa wazee, Ramadhan Salehe akitoa neno la shukrani.
Wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kutoka kampuni ya Barrick
Wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kutoka kampuni ya Barrick.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin