Familia moja imeachwa na uchungu baada ya binti yao kupooza kiakili na kimwili siku ya harusi yake.
Wakizungumza na Afrimax, familia ya Faina, mwenye umri wa miaka 38 kutoka Rwanda, ilisema kuwa aliondoka nyumbani kwenda mjini kutafuta kazi baada ya kushindwa kumaliza shule kwa kukosa karo.
Baada ya kupata kazi ya kuwa kijakazi, alikuwa ndiye wa kutegemewa kuwachamia mkate na baadaye alikutana na mwanaume, na wakapendana.
Walianza kupanga harusi yao, hivyo akarudi kijijini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho, na hapo ndipo mambo yakaanza kwenda mrama.
Faina agonjeka na harusi kufutwa.
Nzanzurwimo Kaitan, baba yake Faina, alisema jambo lisilo la kawaida lilitokea siku ya harusi.
Bibi harusi wa wakati huo akiwa na umri wa miaka 20, alianza kulalamika kuhisi mgonjwa.
"Alianza kuumwa na kichwa, akahisi kizunguzungu na akaanza kuwa na wazimu mitaani. Faina hakuweza kuzungumza na kutembea, hivyo akaanza kutambaa.”
Harusi ikasitishwa, Faina akapelekwa hospitalini, akapata nafuu.
Lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi, na miguu yake ikakunjana, hivyo alishindwa kutembea.
Dada yake mkubwa, Alphonsine, alisema alishuku nguvu za giza zilisababisha janga hilo.
Mchumba wa Faina alingoja kwa miaka mitatu, lakini baadaye alikata tamaa na kumuoa mwanamke mwingine na kujaliwa watoto watatu.
Faina hutumia muda mwingi akiwa nyumbani kwa sababu hawezi kutembea, na familia yake sasa inaomba msaada wa kifedha ili kumnunulia kiti cha magurudumu.