Binti Eurélia Manuel Benjamim Raia wa Msumbiji ambaye alidhaniwa kuwa amefariki dunia na ambaye mazishi yake yalifanyika mwezi Novemba mwaka jana ametokea kijijini kwao Lindi nchini Msumbiji.
Eurélia Manuel Benjamim anatajwa kama Mtu aliyefufuka kutoka kwa wafu lakini yeye mwenyewe anasema alikuwa ameenda tu kufanya kazi katika shamba la Mjomba wake kwa miezi michache.
Msimamizi wa eneo katika Wilaya ya Montepuez amesema Walifanya sherehe zote za mazishi, sherehe ya siku ya tatu na kutembelea kaburi na kaburi halijavunjwa.”
Kikosi cha wataalamu kinatumwa kwenye Kijiji cha Lindi nchini humo kufanya uchunguzi ili kuona ni nani au nini kilizikwa kaburini.
Social Plugin