Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MCHORAJI KATUNI MAARUFU MASOUD KIPANYA ABUNI GARI LA KUCHAJI KWA UMEME


Mchoraji katuni wa Tanzania, Masoud Kipanya amezindua rasmi gari lake ambalo ni la kwanza la umeme kutengenezwa hapa nchini.

Katika Uzinduzi huo uliofanyika jana April 02, 2022 katika Hoteli ya Dar es Salaam Serena na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara nchini. Kipanya amesema gari hilo ni aina ya KP A72eV na linatumia Nishati ya umeme.

Amesema kuwa wazo lake binafsi la ubunifu ambalo lilimchukua miezi 11 kukamilika.

Gari hilo ambalo ni rafiki kwa mazingira kwa sababu halitumii nishati ya mafuta linaitwa Kaypee Motor na linachajiwa kwa saa sita kabla ya kutumika.

"Hili ni gari la nguvu sana ambalo ukinunua unapata na chaji yake," ameongeza Kipanya

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com