SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah katika Viwanja vya Kololo, Jijini Kampala nchini Uganda.
Marehemu Jacob alifariki dunia Machi 20, 2022 nchini Marekani, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kabla ya kufariki Spika huyo wa Bunge la Uganda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa na japo kifo chake kimeacha sintofahamu kutokana na taarifa kuwa alipewa sumu, taarifa ambayo imethibitishwa na baba yake Nathan Okori.
“Najua wote mliokuja hapa kwenye kuomboleza taarifa za kifo chake siyo nyepesi kuzipokea kwasababu najua hakufa kwa kifo cha kawaida aliwekewa sumu",alisema Okori
Social Plugin