Msanii Maunda Zorro enzi za uhai wake
Mwimbaji wa Bongofleva, Maunda Zorro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 14, 2022. Chanzo cha kifo chake ni ajali ya gari.
Ndugu wa damu wa Maunda Zorro msanii wa Bongofleva Banana Zorro amethibitisha kutokea kwa msiba wa mdogo wake.
Msanii Banana Zorro ametoa taarifa ya kinachondelea kwenye msiba wa dada yake Maunda Zorro kwa kueleza kwamba kwa sasa msiba upo Maweni Kigamboni kwa Mzee Zorro na taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa baadaye.
Taarifa ya Maunda Zorro kufariki dunia zimetoka usiku wa kuamkia leo huku chanzo cha kifo chake ni ajali ya gari iliyotokea Kigamboni Dar es Salaam.
Picha ya aliyekuwa msanii Maunda Zorro
Social Plugin