Mwanaume mmoja huko nchini Marekani David Riston, ambaye alikutwa amefariki ndani ya nyumba yake imegundulika kuwa alikuwa mfugaji wa nyoka na kifo chake kimesababishwa na kuumwa na nyoka aliokuwa anawafuga.
Uchunguzi wa Polisi umebaini nyoka zaidi ya 120 ndani ya nyumba yake huku mwili wake ukibainika kuwa na sumu kali ya nyoka hao.
Maafisa wa Ofisi ya Mkaguzi wa Matibabu wa Jimbo la Maryland wamethibitisha kwamba David Riston, (49), alikufa kutokana na kuumwa na nyoka.
Polisi walifanya ukaguzi baada ya jirani wa Riston kuonyesha wasiwasi kwamba hakuwa amemuona Riston kwa takriban saa 24.
Baada ya kuukaribia mlango wa mtu huyo, jirani huyo aliona Riston akiwa ameanguka chini.
Maafisa hao walipokuwa wakiendelea kuingia ndani ya nyumba hiyo, zaidi ya nyoka 100 wenye sumu na wasio na sumu wa aina tofauti waligunduliwa kwenye nyumba hiyo.
Social Plugin