.Mfanyakazi wa Barrick North Mara akionyesha zoezi la kuzima moto
Mafunzo hayo pia yamewafikia wafanyakazi wa baa ya Bambalaga.
Mafunzo hayo pia yamewafikia wafanyakazi wa baa ya Bambalaga.
Mkuu wa idara ya Afya na Usalama wa Mahali pa Kazi wa mgodi wa Barrick North Mara ,Dk.Nicholas Mboya akimkabidhi msaada wa vifaa vya kuzima moto ,Mkuu wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoa wa Dodoma, ACP Anania Amo
Mkuu wa idara ya Afya na Usalama wa Mahali pa Kazi wa mgodi wa Barrick North Mara ,Dk.Nicholas Mboya akimkabidhi msaada wa vifaa vya kuzima moto ,Mkuu wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoa wa Dodoma, ACP Anania Amo
Waendesha bodaboda wa Dodoma pia wamefikiwa na elimu ya kudhibiti majanga ya moto
Mfanyakazi wa Barrick North Mara,Samwel Nyansika akitoa elimu kwa Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) mjini Dodoma.
***
Mgodi wa Barrick North Mara, umetumia fursa ya maonyesho ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi yanayoendelea mkoani Dodoma, kwa kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa taasisi za Serikali na makundi mbalimbali ya jamii sambamba na kugawa vifaa mbalimbali vya kudhibiti moto.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama wa Mahali pa Kazi wa mgodi huo, Dk.Nicholas Mboya, alisema kampuni kwa kutumia wataalamu wake imejipanga kuhakikisha inafikisha elimu hii kwa kuwafuata walengwa katika maeneo yao badala ya kusubiri watembelee banda lao la maonyesho.
Alisema tangu maonyesho yaanze tayari wametembelea na kutoa elimu na kugawa vifaa kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia,madereva wa magari makubwa na bodaboda pia watatembelea sehemu za kumbi za starehe zinazotembelewa na watu wengi ,masoko, shule za Sekondari na vyuo.
“Timu yetu imejipanga, wapo wafanyakazi wanaoelimisha Wananchi kuhusu uendeshaji wa shughuli za Twiga na Barrick nchini kwenye banda letu la maonyesho na wengine wanatoa elimu ya usalama na udhibiti majanga ya moto kwenye jamii” ,alisema Dk.Mboya.
Kwa upande wao baadhi ya taasisi ambazo zimetembelewa na kupatiwa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto na kupatiwa vifaa zimeishukuru kampuni ya Barrick kwa kufikisha elimu hii kwenye jamii.
Mkuu wa kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoani Dodoma, ACP Anania Amo, alishukuru Barrick, baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kuzima moto na sanduku la huduma ya kwanza “Tunawashukuru kwa kututembea ,kutupatia elimu na vifaa hususani katika kipindi hiki ambacho majanga ya moto yamekuwa yakijtokeza mara kwa mara”,alisema ACP Amo.
Naye Meneja msimamizi wa baa ya Bambalaga ,Philipina Focus, alishukuru kwa kupatiwa vifaa na elimu ya kuzima moto na kutoa wito kwa wataalamu wa masuala ya usalama kuendesha mafunzo kwa wananchi kwa kuwa wengi wao licha ya kwamba wanakuwa na vifaa vya kudhibiti moto wanaviona kama mapambo tu hawajui jinsi ya kuvitumia.