OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) imepata kibali cha ajira za Watumishi wa Kada za Afya 7,612 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Ualimu 9,800 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 20 Aprili - 04 Mei, 2022.
Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).
A: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA UALIMU
Walimu wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz.
Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2021. Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo wa maombi ya ajira wanatakiwa kuomba upya.
1.0 SIFA ZA WAOMBAJI
1.1 SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI
Walimu wanaotakiwa kutuma maombi wawe na sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:
1.2 WALIMU WA SHULE ZA MSINGI
Walimu wanaoomba kuajiriwa kufundisha Shule za Msingi wawe na sifa zifuatazo:
i. Mwalimu Daraja la III A - Mwenye Astashahada ya Ualimu Elimu ya
Msingi (Certificate in Primary Education);
ii. Mwalimu Daraja la III B - Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Awali;
iii. Mwalimu Daraja la III B - Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Msingi;
iv. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu kwa Elimu ya
Awali; na
v. Mwalimu Daraja la III A, III B na III C – Mwenye Astashahada,Stashahada na Shahada ya Ualimu (Elimu Maalum) kwa masomo ya Lugha na Sanaa.
1.3 WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI
i. Mwalimu Daraja la III B - Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu Maalum kwa masomo ya English Language, Geography, History, Kiswahili, Biology, Chemistry, Physics na Mathematics;
ii. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu aliyesomea Elimu Maalum kwa masomo ya English Language, Geography, History, Kiswahili, Biology, Chemistry, Physics na Mathematics;
iii. Mwalimu Daraja la III B - Mwenye Stashahada ya Ualimu wa somo la Biology, Chemistry, Physics na Basic Mathematics;
iv. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu somo la Physics,Mathematics, Chemistry na Biology;
v. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu wa somo la English Language, English Literature, Chinese Language, French Language na Kiswahili;
vi. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu somo la Commerce, Accountancy na Economics;
vii. Mwalimu Daraja la III B - Mwenye Stashahada ya Ualimu Elimu somo la
Book Keeping na Commerce;
viii. Mwalimu Daraja la III C - Mwenye Shahada ya Ualimu kwa masomo ya
General Studies, History na Geography;
ix. Mwalimu Daraja la III B - Mwenye Stashahada ya Ualimu kwa masomo
ya Civics, History, Geography, English Language na Kiswahili;
x. Mwalimu Daraja la III C – Mwenye Shahada ya Elimu ya Michezo
(Bachelor of Science in/ with Physical Education); na
xi. Mwalimu Daraja la III B - Mwenye Stashahada ya Elimu ya Michezo
(Diploma in Physical Education).
B: TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA KADA ZA AFYA
Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia
kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Waombaji ambao waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo wa maombi ya ajira wanatakiwa kuomba upya.
2.0 Sifa za Waombaji ni kama ifuatavyo:-
2.1 DAKTARI DARAJA LA II
Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Waombaji wawe wamemalizamafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
2.2 DAKTARI WA MENO DARAJA LA II
Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
2.3 TABIBU DARAJA LA II
Waombaji wawe na Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.4 TABIBU WA MENO DARAJA LA II
Waombaji wawe na Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma in Clinical Dentistry) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.5 TABIBU MSAIDIZI
Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili ya Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant Certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.6 MFAMASIA DARAJA LA II
Waombaji wawe na Shahada ya Famasi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).
2.7 MTEKNOLOJIA (DAWA) DARAJA II
Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Dawa (Diploma in Pharmaceutical Technology) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).
2.8 MTEKNOLOJIA (MAABARA) DARAJA II
Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Diploma in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
2.9 MTEKNOLOJIA MSAIDIZI (MAABARA)
Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
2.10 MTEKNOLOJIA (MIONZI) DARAJA II
Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Mionzi (Diploma in Radiology/Radiography) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wawe wamesajiliwa na Baraza la
Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging
Professionals Council)
2.11 AFISA MUUGUZI DARAJA LA II
Waombaji wawe na Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo kwa vitendo (Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurses and Midwifery Council).
2.12 AFISA MUUGUZI MSAIDIZI DARAJA LA II
Waombaji wawe na Stashahada ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).
2.13 MUUGUZI DARAJA LA II
Waombaji wawe na cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la
Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council)
2.14 FUNDI SANIFU VIFAA TIBA II
Waombaji wawe na Stashahada ya kawaida ya Ufundi (Full Technician Certificate) ya miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.15 AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA II
Waombaji wawe na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Afya ya Mazingira (The Environmental Health Practitioners’ Registration Council).
2.16 MSAIDIZI WA AFYA
Waombaji wawe wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu Mafunzo ya Mwaka mmoja katika fani ya Afya, Afya Ngazi ya Jamii au mafunzo yoyote yanayofanana na hayo kutoka vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali.
2.17 KATIBU WA AFYA DARAJA LA II
Waombaji wawe na Shahada ya Uongozi wa Huduma za Afya (Health Services Administration) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
2.18 AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II
Waombaji wawe na Shahada au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Social Work, Sociology, Psychology, Social Protection, Guidance and Counceling, Theology, Divinity, Child Protection, Social Policy, Early Childhood Development, Social Gerontology, Dietetics au fani nyingine zinazofanana na Ustawi wa Jamii kutoka Chuo cha Elimu ya Juu kinachotambuliwa na Serikali.
.19 AFISA LISHE DARAJA LA II
Waombaji wawe na Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc - Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and Technology, Food Science) au Stashahada ya Juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka Chuo cha Elimu ya Juu kinachotambuliwa na Serikali.
3.0 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI
i. Awe raia wa Tanzania;
ii. Awe na umri usiozidi miaka 45;
iii. Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha
Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya
kufanya kazi ya taaluma husika);
Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya
Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
v. Waombaji walioajiriwa kwa mkataba wa ajira kutoka kwa Wadau wa
Maendeleo katika Sekta ya Afya wanatakiwa kuambatisha nakala za
mkataba na barua za uthibitisho kutoka kwa Wakurugenzi wa
Halmashauri husika;
vi. Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi
wa Umma;
vii. Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIN); na
viii. Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
4.0 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE
i. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika Halmashauri/Vituo
watakavyopangiwa;
ii. Waombaji wawe tayari kufanya kazi na Mashirika au Taasisi zilizoingia
Ubia na Serikali;
iii. Baada ya kupangiwa kituo cha kazi, hakutakuwa na nafasi ya
kubadilishiwa kituo cha kazi;
iv. Waombaji wote wahakikishe wanajaza taarifa zao na kuambatisha
nyaraka zote muhimu katika mfumo; na
v. Maombi ya ajira ni bure.
5.0 WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI
i. Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ... kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezesha kuingia kwenye Mfumo wa Ajira; na
ii. Waombaji waliosoma Vyuo vya Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati ya
masomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyao
viweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa nchini.
Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa
maombi kwa nafasi za Kada za Afya na Elimu, tafadhali bofya: www.tamisemi.go.tz au
wasiliana na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba
za simu 026 2160210 au 0735 160210.
Waombaji wenye Ulemavu na sifa zilizoainishwa katika tangazo hili watume
maombi yao ya kazi kwa nakala ngumu (hard copy). Maombi yao yaeleze aina ya
ulemavu wao na kuambatisha picha zao na yatumwe katika anwani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira & Wenye Ulemavu)
S.L.P.980,40480 DODOMA (Aione: Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye
Ulemavu)
Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa
moja Ofisini hayatafanyiwa kazi. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe
04 Mei, 2022 saa 05:59 usiku. Tangazo hili linapatikana katika tovuti ifuatayo:
Limetolewa na: Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais - TAMISEMI,
Mji wa Serikali - Mtumba,
S.L.P 1923,
41185 DODOMA.
Aprili 20,2022.
Unaweza kupakua PDF <<hapa>>
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com