Picha : POLISI SHINYANGA, WAANDISHI WA HABARI WAENDESHA MDAHALO NAMNA YA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP George Kyando akizungumza kwenye mdahalo wa waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KLABU ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (SPC), wamefanya mdahalo na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, katika kujadiliana namna ya kuimarisha mahusiano mazuri na Jeshi hilo hasa wanapokutana kwenye matukio na kila mmoja akitekeleza majukumu yake na kusiwepo na mifarakano pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama kwa pande zote.

Mdahalo huo umefanyika leo Aprili 28, 2022 kwa kukutanisha maofisa wa Jeshi la Polisi ngazi za juu mkoani Shinyanga, pamoja na waandishi wa habari mkoani humo.

 Akizungumza wakati wa kufungua Mdahalo huo,Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Patrick Mabula, amesema Jeshi la Polisi na waandishi wa habari wanapaswa kuwa na mahusiano mazuri, kwa sababu wanategemeana katika utekelezaji wa majukumu hasa katika matukio ya kiharifu na ajali za barabarani.

“Lengo kubwa la mdahalo huu ni kuboresha mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari hasa katika utekelezaji wa majukumu yetu,”amesema Mabula.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP George Kyando, amepongeza kufanyika kwa mdahalo huo na kueleza kuwa ni muhimu sana katika kuimarisha mahusiano mazuri baina ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari.

“Waandishi wa habari na Jeshi la Polisi wanafanya kazi sawa, sababu nyie mnategemea kupata taarifa za uhalifu kutoka Jeshi la Polisi na kwenda kuhabarisha umma, na kutusaidia sisi kupunguza uharifu au kuukomesha kabisa kupitia kalamu zenu,”amesema Kyando.

“Nawapongeza sana walioandaa mdahalo huu, ambao ni muhimu sana katika kuimarisha mahusiano mazuri baina ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari, kwa sababu nyie mnafanya kazi sawa na sisi hasa katika kuhabarisha umma juu ya matukio ya uhalifu na kuacha mara moja,”ameongeza.

Katika hatua nyingine Kamanda wa Jeshi la Polisi, amewataka waandishi wa habari mkoani humo, kujenga tabia ya kufika kwenye maeneo ya matukio hasa yale ya karibu, na siyo kutegemea kila kitu kutoka kwa Jeshi la Polisi na kushindwa kupata taarifa ya tukio kwa undani zaidi.

Amesema Jeshi la Polisi linapofika kwenye tukio, huwa halikusanyi taarifa za habari, bali wao huwa wanafika kukusanya ushahidi wa tukio, na kuwataka wabadilike katika utendaji wao kazi wa kukusanya taarifa na kuhabarisha umma.

“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tupo pamoja kushirikiana na ninyi waandishi wa habari katika utekelezaji wa majukumu yenu, lakini kwa kuzingatia taratibu na kazi zetu, na pia mbalansi habari zenu hasa za matukio,”amesema Kyando.

Naye Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Shinyanga (RTO) Debora Lukololo, amesema ili waandishi wa habari kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi ni lazima wafanye kazi zao kwa weledi pamoja na kubalansi taarifa zao na kupata usahihi wa tukio na siyo kulirusha na kuleta taharuki.

Nao baadhi ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga, wamesema mdhahalo huo umesaidia kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri baina ya waandishi wa habari na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP  George Kyando, akizungumza kwenye mdahalo huo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando akizungumza kwenye mdahalo huo.

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Patrick Mabula, akizungumza kwenye mdahalo huo.

Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani mkoani Shinyanga Debora Lukololo akizungumza kwenye mdahalo huo.

Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani mkoani Shinyanga Analyse Kaika akizungumza kwenye mdahalo huo.

Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Ally Litwayi, akizungumza kwenye mdahalo huo.

Mjumbe wa Kamati Tendaji Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Marco Mipawa, akichokoza mada kwenye mdahalo huo.

Mjumbe wa Kamati Tendaji Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Marco Mipawa akichangia mada kwenye mdahalo huo.

Mwandishi wa Habari AZAM TV Kosta Kasisi akichangia Mada kwenye mdahalo huo.

Mkurugenzi mtendaji wa Malunde 1 blog Kadama Malunde akichangia hoja kwenye mdahalo huo.

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe wilayani Kahama Shabani Njia, akichangia hoja kwenye mdahalo huo.

Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Mwandishi wa Nipashe wilayani Kahama Shabani Njia akiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mdahalo huo.

Viongozi na wajumbe wa Kamati Tendaji Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo George Kyando na maofisa wa Jeshi hilo mkoani Shinyanga.

Viongozi na wajumbe wa Kamati Tendaji Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo George Kyando na maofisa wa Jeshi hilo mkoani Shinyanga.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post