Paul Hendrik van Zyl (77) ambaye ni raia wa Afrika kusini mwenye asili ya weupe amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumpiga risasi mwanamke mweusi Ramokone Linah aliyekuwa katika shamba la mwanaume huyo na kudai kuwa alidhani ni mnyama aina ya Kiboko.
Ramokone Linah mwenye umri wa miaka thelathini na nane alipata majeraha ya risasi kwenye mkono wake, wakati mpenzi wake aliyekuwa naye shambani hapo akifanikiwa kujiicha.
Polisi nchini Afrika Kusini wanasema Mshtakiwa huyo ndiye mmiliki wa shamba ambalo tukio lilitokea.
Hendrik aliachiliwa kwa dhamana ya randi 1,000 (dola 62) na kesi imeahirishwa kwa uchunguzi zaidi hadi Mei 18.
Kundi la wafuasi wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto wa Economic Freedom Fighters (EFF) wameonyesha kutokurishishwa na mtuhumiwa huyo kupewa dhamana
Social Plugin