LATRA YATANGAZA NAULI MPYA ZA DALADALA NA MABASI YAENDAYO MIKOANI


Mamlaka ya udhibiti wa usafiri Ardhini LATRA imetangaza viwango vipya vya bei ya nauli za daladala na mabasi ya mikoani huku nauli ya daladala kwa wanafunzi ndio nauli iliyobaki kama ilivyokuwa.

Akitangaza viwango hivyo Mkurugenzi wa LATRA Gillard Ngewe amebainisha kuwa viwango hivyo vipya vya nauli vitaanza kutumika May 14, 2022, huku nauli iliyokuwa shilingi 400 ikiongeka na kuwa shilingi 500.

Ngewe amefafanua kuwa kwa sasa umbali wa Kilometa 0 – Kilometa 10 nauli yake ilikuwa shilingi 400 sasa hivi itakuwa shilingi 500, umbali wa Kilometa 15 nauli kwa sasa itakuwa shilingi 550, umbali wa Kilometa 20 nauli itakuwa shilingi 600, Kilometa 25 Nauli itakuwa shilingi 700 na kwa Kilometa 30 nauli itakuwa shilingi 850.

Haya yanajiri katika kipindi hiki ambapo bei ya mafuta imepanda, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, inayoathiri pia uchumi wa dunia.

CHANZO- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post