Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa Mwanza limeendesha kongamano la 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' kwa waumini wa dini ya kiislamu wilayani Sengerema kwa lengo la kuimarisha amani katika familia hususani kwa wanandoa.
Kongamano hilo limefanyika Jumatatu Aprili 25, 2022 katika msikiti wa wilaya Sengerema ikiwa ni mwendelezo wa makongamano ya aina hiyo yaliyoandaliwa na BAKWATA Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na shirika la KIVULINI katika wilaya zote mkoani Mwanza.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke amesema elimu inayotolewa kupitia makongamano hayo itasaidia kurejesha maadili katika jamii hususani kunusuru wimbi la ndoa zinazofungwa mwezi wa Shaabani na kuvunjika baada ya mwezi wa Ramadhani.
Katika hatua nyingine Sheikh Kabeke amewahimiza wazazi kufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto wao ili kutengeneza kizazi cha wataalam watakaosaidia usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya inayoanzishwa na BAKWATA.
Washiriki katika kongamano hilo wameomba kuwa endelevu na si kuishia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwani elimu inayotolewa itasaidia kuponya ndoa nyingi na kuondokana na matendo yasiyofaa ambayo yamekuwa yakichangia mifarakano miongoni mwa wanandoa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akizungumza kwenye kongamano la 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' lililofanyika katika msikiti wa Wilaya Sengerema.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akisisitiza jamii kurejea misingi ya dini, kuishi kwa maridhiano katika ndoa hatua itakayosaidia ndoa kudumu kuondokana na changamoto ya watoto kukosa malezi ya wazazi wa pande zote, mme na mke.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke (kushoto) akizungumza kwenye kongamano hilo. Kulia ni Sheikh Twaha Bakari ambaye ni Msaidizi wa Sheikh wa Mkoa Mwanza.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Sengerema wakifuatilia mawaidha kutoka kwa Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke wakati wa kongamano 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' lililofanyika katika msikiti wa Masjid Munawwara.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Sengerema wakifuatilia kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Sengerema wakifuatilia kongamano maadili lililoandaliwa na BAKWATA Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na shirika la KIVULINI ili kurejesha maadili katika jamii.
Waumini wa dini ya kiislamu wakifuatilia kongamano hilo ambapo BAKWATA Mkoa Mwanza inatumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuelimisha umma kurejea kwenye maadili na misingi ya dini ili kuondokana na ukatili wa kijinsia katika familia.
Waumini wa dini ya kiislamu wakifuatilia kongamano hilo.