Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Zanzibar, Khamis Abdallah Said akizungumza wakati akifungua kongamono la kuwajengea uwezo vijana kupata fursa za ajira, lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini (AIESEC) kwa kushirikiana na Benki ya CRDB, lililofanyika mwishoni wa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Michenzani, Unguja Zanzibar. kushoto ni Rais wa Umoja wa Taasisi za Elimu ya juu za wanafunzi nchini Tanzania (AIESEC), Furaha Alphone.
Meneja wa Mafunzo na Maendeleo ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB, Edith Mwiyombela akizungumza na wanafunzi wa Vyuo vikuu Visiwani Zanzibar waliohudhuria kongamano hilo.
Benki ya CRDB kwa mara nyingine imeshiriki katika Kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo Vikuu na kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuongozi pindi wamalizapo masomo, lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Michenzani, Unguja Zanzibar, ikiwa ni mwendelezo baada ya lile lililofanyika Dar es salaam katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) majuma kadhaa yaliyopita.
Benki ya CRDB imekuwa ni moja ya benki kiongozi nchini katika kuhakikisha inashiriki kuelimisha makundi ya vijana wa vyuo mbalimbali nchini kupitia program mbalimbali yakiwemo Mafunzo kwa vitendo ‘Field attachmets’, Mafunzo kazini 'Ínternship’ na Programu maalumu ya Maendeleo ya wahitimu ‘Apprenticeship’ ambayo yalianzishwa mwaka 2020 kwa kuwachukua wahitimu 29 kutoka nchini Tanzania na 2 kutoka nchini Burundi.
Pia Benki ya CRDB kila mwaka huchukua kati ya wanafunzi 300 hadi 500 na kuwaunganisha katika vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya benki hiyo na kwenye matawi yake yaliyosambaa kote nchini ilikuweza kuwapatia mafunzo ya vitendo.
Wanafunzi wa vyuo nchini wamekuwa wakifurahia huduma mbalimbali za kibenki kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni pamoja na upatikananji wa mikopo maarufu kama Boom Advance umekuwa ni mkombozi kwa wanafunzi wengi wanaotumia benki ya CRDB kwakujipatia mikopo rahisi hivyo kurahisisha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kifedha. Pia Benki ya CRDB imewatengenezea akaunti maalumu ya wanafunzi wa vyuo ambayo gharama zake za kufungua akaunti hiyo ni shilingi za Kitanzania Elfu Tano tu (5,000). wastani wa mikopo 20,000 inatolewa kila Mwezi kwa wanafunzi mbalimbali nchini, na wastani wa akaunti 50,000 zinafunguliwa kila mwaka na wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini.
Kwa miaka mitano sasa Benki ya CRDB imekuwa Mshirika wa Umoja wa Taasisi za Elimu ya juu za wanafunzi nchini Tanzania ‘AIESEC’.
Social Plugin