Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AJIUA BAADA YA KUVAMIA SHULE NA KUUA WANAFUNZI NA MWALIMU WAO

Ruslan Akhtyamov mwenye umri wa miaka 26 amewaua watoto wawili wa shule ya awali pamoja na Mwalimu wao

***
RAIA mmoja nchini Urusi anayefahamika kwa jina la Ruslan Akhtyamov mwenye umri wa miaka 26 amevamia shule moja ya wali nchini Urusi akiwa na bunduki na kufyatua risasi iliyomuangamiza mwalimu wa shule hiyo huku bila huruma akiwafyatulia risasi watoto wawili kabla ya yeye mwenyewe kujimaliza.


Mwalimu huyo aliyefahamika kwa jina la Olga Mitrofanova alikuwa ni mstaafu anayefundisha shule ya awali ya watoto ambao watoto wawili waliofariki ni wenye umri wa miaka mitano na sita katika mji wa Ulyanovsk uliopo nchini Urusi.


Taarifa zinadai kuwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo Ruslan alikuwa tayari amekwisha muua jirani yake aliyefahamika kwa jina la Alexander Dronin mwenye umri wa miaka 68.


Mwalimu huyo aliuawa akiwa katika harakati za kumzuia muuaji huyo asiingie ndani kuwadhuru watoto, miili ya watoto hao ilifahamika kwa majina ya Vladimir Vova Krylov mtoto mwenye umri wa miaka mitano na Ekaterina Katya Sosnova mwenye umri wa miaka sita.

Eneo la tukio ambapo uchunguzi bado unaendelea

Hadi sasa sababu za mauaji hayo hazijafahamika huku ikibainika kuwa muuaji alikuwa na bunduki aina ya IZH-27 aliyokuwa anaimiliki kihalali ikiwa na leseni ya uwindaji.


Shuhuda wa mauaji hayo ambaye ni mama mlezi wa watoto katika shule hiyo anayefahamika kwa jina la Elena Karpova mwenye umri wa miaka 52 ambaye katika tukio hilo alijeruhiwa mkono.


“Mwanaume mwenye bunduki aliingia ndani katika muda ambao ulikuwa umetulia kabisa akawapiga risasi watoto wawili pamoja na mwalimu kisha akajiua.”


Taratibu za uchunguzi bado zinaendelea huku taarifa za awali zikibainisha kuwa mauaji hayo yanaweza kuwa yamesababishwa na migogoro ya kifamilia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com