Msanii wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz.
**
DIAMOND Platnumz; ni msanii mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na Kusini mwa Jangwa la Sahara ambaye amepata pigo kubwa baada ya chaneli yake ya Mtandao wa YouTube kufutwa.
Kwa sasa ukiitembelea chaneli yake hiyo kwa jina la Diamond Platnumz hakuna kitu chochote zaidi ya maelezo kwamba chaneli hiyo imefutwa kutokana na kukiuka kanuni za mtandao huo.
Hii ni hasara kubwa kwa Diamond kwa sababu chaneli yake ndiyo kubwa na yenye wafuasi (subscribers) zaidi ya milioni 6.3 ambayo kama nyimbo zote zimefutwa, basi zile rekodi za kuwa na mabilioni ya watazamaji zinaenda kufutika na kupoteza mamilioni ya pesa.
Kilichotokea leo, ni siku mbili baada ya chaneli hiyo kudukuliwa ambapo timu ya digital ya Diamond ilifanya kazi kubwa kuirejesha
Social Plugin