Mhandisi Kilimo kutoka kituo cha CAMARTEC Godrey Mwinama akionesha baadhi ya zana ambazo zinatengenezwa katika kituo hicho
Na Rose Jackson,Arusha
Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia vijijini CAMARTEC wameishukuru Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia kwa kuwa wadau muhimu wa kuwapatia fedha za ubunifu na uendelezaji wa teknolojia vijijini.
Akizungumza na waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo na COSTECH Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho kwa lengo la kujifunza habari za matokeo ya sayansi na utafiti mhandisi kilimo kutoka CAMARTEC Godfrey Mwinama amesema kuwa COSTECH wamekuwa na mchango mkubwa katika kituo hicho.
Aliongeza kuwa kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imewezesha kuibua zaidi ya bunifu mia moja ambapo COSTECH imekuwa ikiwapatia fedha kwa ajili ya kuendeleza bunifu hizo.
"Kuna trekta ambalo linatengenezwa hapa CAMARTEC na fedha zake tumepewa na COSTECH hivyo tunakiri kuwa wamekuwa bega kwa bega na sisi kuhakikisha kuwa tunazalisha teknolojia ambazo zinaweza kuwafikia wananchi na wadau mbali mbali",alisisitiza Mwinama.
Naye Kaimu Meneja wa uzalishaji wa CAMARTEC Mhandisi Boniface Masawe amesema kuwa kituo hicho kimefanikiwa kubuni na kutengeneza jiko la mfumo jua ambalo Lina uwezo wa kutumika kipindi Cha kiangazi na hivyo kuweza kuokoa matumizi ya gesi na umeme.
Masawe amesema kuwa jiko hilo lina uwezo wa kufyonza mionzi ya jua na kukusanya sehemu moja kwa ajili ya kupika.
"Jiko hili ni rahisi kwenye maeneo ambayo yana jua la kutosha kwani linatumia mionzi ya jua ambapo pia Lina uwezo wa kudumu muda mrefu kwa kuwa sio la kuhamisha hamisha likishafungiwa sehemu moja halihamishwi tena",aliongeza Masawe.
Amesema kuwa jiko hilo ni rahisi na limekuwa likifanya vizuri kwa mikoa ya Singida na Dodoma na Lina uwezo wa kupika maharagwe kwa dakika 45 na hivyo kuweza kuokoa gharama nyingine za nishati ya gesi.
Social Plugin