KATAMBI AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini akizungumza kwenye futari hiyo.

Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, amewaomba viongozi wa dini mkoani Shinyanga, kuliombea Taifa amani na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassani afya njema ili aendelee kuitumikia nchi na kuleta maendeleo.

Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, alibainisha hayo jana wakati akishiriki futari iliyoiandaa kwa viongozi wa dini ya kiislamu mkoani Shinyanga.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassani ameichukua nchi katika kipindi kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Rais Hayati John Magufuli, hivyo watanzania wanapaswa kumuunga mkono katika majukumu yake ya kuwaletea maendeleo, pamoja na viongozi wa dini kuliombea Taifa amani na Rais Samia kuendelea kuwa na afya njema.

“Nawaomba viongozi wa dini tuendelee kuliombea Taifa letu amani na kumuombea Rais Samia Afya njema ambaye anafanya kazi kubwa ya kutuletea maendeleo na ameichukua hii nchi katika kipindi kigumu, hivyo tumuunge mkono kwa kila hatua ambayo anaipiga,”alisema Katambi.

Naye Naibu Waziri wa Afya Dk, Godwin Mollel, ambaye alishiriki Futari hiyo, alisema mataifa mengi ambayo yameendelea yamemtanguliza mwenyezi Mungu mbele, na kuwaomba watanzania kila jambo wanalolifanya wasimsahau mwenyezi mungu sababu yeye ndiyo ufunguo wa kila kitu.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habib Makusanya, alisema anashukuru viongozi hao kujumuika kula nao futari, huku wakiahidi kuwa wataendelea kuliombea taifa amani na kuuombea Rais Samia Suluhu Hassani aendelea kuwa na afya njema ili awatumikie vizuri.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini akizungumza kwenye Futari hiyo.

Naibu Waziri wa Afya Dk, Godwin Mollel, akizungumza kwenye Futari hiyo.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye Futari hiyo.

Viongozi wa dini wakiwa kwenye Futari hiyo.

Viongozi wakishiriki Futari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akishiriki Futari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post