Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ACP Maketi Msangi
Na Mbuke Shilagi -Kagera
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Stide Joackim (34) mkazi wa kijiji Kyaka kata Kyaka Wilaya ya Misenyi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka 16.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ACP Maketi Msangi amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo mnamo tarehe 18 Aprili mwaka huu majira ya saa 5:30 usiku katika kijiji cha Kyaka kata ya Kyaka wilayani humo, na mnamo tarehe 20 Aprili mwaka huu majira ya saa 8:30 mchana alikamatwa akiwa katika kijiji cha Bulfani pia kilichopo katika kata hiyo.
ACP Msangi amesema kuwa, chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mwili na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu, ili hatua zichukuliwe kabla ya madhara kutokea.
Social Plugin