Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Carolyne Nombo akizungumza wakati akifunga mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo. Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Carolyne Nombo akiwa katika ufungaji wa mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba akiwa katika ufungaji wa mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo. Walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce wakiwa katika ufungaji wa mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu hao yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo. Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Carolyne Nombo akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba wakipata picha ya pamoja na walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce wakati wa ufungaji wa mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo.
************************
NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Carolyne Nombo leo Aprili 13,2022 amefunga mafunzo ya walimu Kazini kwa walimu wa masomo ya Book Keeping na Commerce yaliyofanyika kwa siku sita katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) wilayani Bagamoyo.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo, Prof.Nombo amesema kuna umhumu mkubwa kupitia mafnzo hayo yakatumike kwa vitendo na matokeo yake yaweze kuonekana.
Amesema kuwa Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuwapatia mafunzo walimu hao ambayo yatawasaidia katika kuhakikisha ufundishaji na upimaji unafanyika vyema kwa wanafunzi ili wawe wataalamu wazuri kwenye masuala ya uhasibu na biashara nchini.
"Mafunzo haya yatatusaidia kuzalisha wataalamu ambao wataleta tija katika manufaa ya nchi yetu, ninaamini yatatusaidia sisi kama jamii kuweza kufikia malengo ya mtu mmoja mmoja na ttaifa kwa ujumla". Amesema Prof.Nombo
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amesema mafunzo hayo yamefadhiliwa na serikali kupitia fedha ya maendeleo zilizotolewa kwa TET katika mwaka wa fedha 2021/22 ambapo TET imepokea jumla ya shilingi Bilioni 1,243,400,000.
Amesema mafunzo hayo yametolewa kwa walimu 451 wa masomo ya Book-Keeping na Commerce kutoka shule za sekondari za serikali na zisizo za serikali Tanzania bara na visiwani na lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuwajengea walimu uwezo wa kufundisha masomo ya michepuo kwa ufanisi mkubwa zaidi.
“Ni imani yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa chachu yakuweza kufikia malengo ya kitaifa yaliyokusudiwa katika nyanja ya biashara nchini hivyo mkayatumie vyema na kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kufanya vizuri katika masomo haya “amesema Dkt.Komba.
Social Plugin