Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAYELE AZIDI KUWA MWIBA, YANGA YAICHAPA NAMUNGO FC 2- 1



*************

YANGA imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya Kutwaa ubingwa wa 28 baada ya kuvunja mwiko wa kutokupata ushindi toka kwa Namungo FC baada ya kuichapa mabao 2-1 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Fiston Mayele dakika ya 17 akipiga tobo mlinda mlango David Mapigano.

Shiza Kichuya aliisawazishia Namungo dakika ya 33 akifunga bao safi kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Yanga Diarra Djigui bao la ushindi kwa Yanga limewekwa kimiani na Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 38.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 54 na kuendelea kujichimbia kilele mwa msimamo wa Ligi hiyo huku wakituma salamu wa watani zao Simba ambao mechi yao dhidi ya watani utapigwa April 30,2022

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com