MIAKA 58 YA MUUNGANO WATUMISHI WA MAKAO MAKUU WILAYA YA MULEBA WAFANYA USAFI KITUO CHA AFYA CHA KAIGARA NA KUTEMBELEA ENEO LA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA

Katikati ni katibu Tawala Wilaya Muleba wakiwa anafanya usafi
Kaimu Mganga mkuu wa Hospital ya Wilaya Muleba Dr. Leontine Rwamulaza akizungumza na waandishi wa Habari.
Picha ya pamoja ya watumishi wa Halimashauri ya Wilaya Muleba.

Watumishi wa Halimashauri ya Wilaya Muleba wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya Muleba

Kulia ni Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya Muleba Elias Kayandabila akiwa katika eneo itakapo jengwa hospitali ya Wilaya.

*********

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Katika maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Watumishi wa Wilaya Muleba wakiongozwa Katibu Tawala Wilaya Ndg. Greyson Mwengu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Elias Kayandabila wamefanya usafi kituo cha Afya Kaigara kisha kutembelea na kukagua eneo litakalojengwa Hospitali ya wilaya inayotarajiwa kuanza kujengwa kuanzia kesho tarehe 27/04/2022 katika eneo la kitongoji cha Malahala, kijiji cha Magata, kata ya Magata Karutanga.

Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua eneo hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Machi, 2022 Halmashauri imepokea kiasi cha Tsh. Milioni 500 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya. Ambapo taratibu zote za manunuzi kwa ajili ya kuanza shughuli ya ujenzi zimekamilika na kuanzia kesho shughuli za ujenzi wa msingi zitaanza rasmi.

"Kwa fedha hizi ambazo tumezipata tunaenda kuanza na ujenzi wa majengo mawili, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la maabara. Naishukuru sana Serikali kuu kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospital yetu ya Wilaya," ameeleza Ndg. Kayandabila.


Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya Dr. Leontine Rwamulaza ameeleza kuwa ujenzi wa Hospitali ya wilaya utasaidia kupunguza changamoto ya huduma ya matibabu kwa wananchi wa Wilaya ya Muleba kwani wataweza kupata huduma za matibabu kwa gharama nafuu ukilinganisha na gharama za hospital binafsi.

Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano kutokea ofisi za makao makuu ya Wilaya (Bomani), usafi kituo cha afya Kaigara kisha eneo itakapojengwa Hospitali ya wilaya kitongoji cha Malahala, kijiji Magata, kata ya Magata Karutanga.

.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post