Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo Dodoma kuhusu msimamo wa kuwahamisha wafanyabiashara wa soko la Sabasaba kupisha ukarabati wenye lengo la kuboresha soko hilo kuwa la kisasa linalokidhi vigezo vya makao makuu ya nchi.
Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA.
LICHA ya wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba Jijini hapa kutishia kuandamana hadi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ili kumfikishia
kilio chao cha kuondolewa katika eneo hilo, Mkurugenzi wa Jiji la
Dodoma Joseph Mafuru ameendelea kuwataka wafanyanishara hao kupisha
ukarabati wa soko hilo huku akieleza lengo la serikali ni jema kwa
maslahi ya wafanyabaishara hao na siyo vinginevyo.
Hayo
yanajiri ikiwa ni hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka
kuagiza Jiji la Dodoma kufanya mkakati wa Uboreshaji wa Soko hilo kwa
kuwaorodhesha wafanyabiasha wote katika mfumo maalum ili kuweza kuondoa
migogoro inayoweza kujitokeza hapo baadaye.
Akiongea
na waandishi wa habari leo Aprili 20, 2022 Ofisini kwake amesema lengo
la Jiji ni kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara hao ili kufanya
ukarabati wa soko hilo na baada ya ujenzi huo kukamilika watawarudisha
kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
"Zoezi
hili tunalifanya kwa uwazi,tuliwashirikisha wafanyabiashara wote na
kilichobaki sasa ni kuhakiki ili kuwatambua nani anamiliki nini na
anafanya nini na kuwaondoa hofu kuwa tunakwenda kuwahamisha kwa muda ili
kupisha ujenzi wa eneo hilo kwa muda wa mwaka mmoja au miwili kulingana
na mchoro wetu”amesema Mafuru
Aidha
amesema soko hilo ni la historia na limechakaa kutokana na kuwa ni la
muda mrefu tangu mwaka 1996 halijafanyiwa ukarabati wa miundominu yake
hivyo ni wakati muafaka wa kuhakikisha linakarabatiwa kisasa zaidi
kulingana na mahitaji na kuweza kuhudumia zaidi ya wafanyabiashara 7000 .
"Lengo
la jiji ni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na si
kuwadhulumu,imefika wakati wafanyabiashara kuelewa Dodoma Sasa ni Jiji
na ndiyo Makao makuu ya nchi na soko la Sabasaba limekuwa halina hadhi
lazima tufanye ukarabati,"amefafanua na kuongeza;
Mvua
ikinyesha pale Sabasaba watu wanashindwa kufanya shughuli zao kwa
utaratibu tope linakuwa la kutisha na nimekuwa nikipokea malalamiko
mengi kuwa tunachukua ushuru lakini hatufanyi ukarabati”amesema Mafuru
Amesema
jiji halina lengo la kuwaonea wafanyabiasahara bali kinachotakiwa ni
kuwashirikisha kila hatua ili kuweza kupata uelewa wa pamoja na kila mtu
kuridhika na maamuzi hayo.
Hata
hivyo amesema malalamiko ambayo wamekuwa wakiyapata yanaonyesha kuwa
wafanyabiashara hao hawana imani na jiji katika kutekeleza mpango huo
hivyo Kutoa nafasi ya kuwahudumia huku akitoa maelekezo kwa wapangaji
waliojimilikisha zaidi ya kibanda kimoja kuwa watamiliki kibanda kimoja
tu ili kuwapa nafasi watu wengine .
"Kuna
baadhi ya wafanyabiashara wamejimilikisha zaidi ya vibanda 20 na
kuvipangisha kwa watu wengine kwa bei ya juu niseme wazi kuwa baada ya
ukarabati huo Kila mfanyabiashara atakuwa na haki ya kumiliki kibada
kimoja ili kila mfanya biashara awe na fursa,"amesema
Naye
Afisa biashara wa Jiji la Dodoma Donatila Vedasto amesema lengo la
kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara ni kupisha uboreshaji wa
miundombinu na kwamba mpango huo ni wa kitambo lakini haukutekelezwa kwa
wakati kutokana na ufinyu wa bajeti uliokuwepo.
Amesema
ili kupata kauli moja wanapanga kuendelea na vikao vya kujadilina baina
ya jiji na uongozo wa soko hilo ili kupata namna bora ya kufikia
mwafaka.
“Kuna watu
wanahofu kupoteza vibanda vyao hasa wale wenye maeneo zaidi ya moja
lakini ni wahakikishie kuwa kupitia mazungumzo tutafikia mwafaka na
hakuna atakaye poteza haki yake waelewe tuu tunafanya uhakiki ili
kujilidhisha na idadi ya wafanyabiasahara iliyopo”amesema
Amesema
"Soko la sababasa miundombini yake imechakaa na hata ukienda sasa hivi
kuko wazi lakini pia hili ni jiji na makao makuu hatuwezi kuwa na soko
la aina ile kama jiji tukasema kuwe na kitu cha kufanya kuboresha soko
kama hadhi ya jiji na kuendana na makao makuu ya nchi,
Tukawaza
kuweka mkakati kwa maana katika mradi huu tutanza ujenzi mwezi wa saba
na huwezi kuanza bila kuwashirikisha wadau ,vikao vimeanza tangu mwaka
jana kuhusiana na changamoto kikubwa miundombinu vikao vya kuanza
kujenza tumeanza mwezi wa kwanza wtaalam walikuja tukawashirikisha,"
amesema Afisa huyo wa Biashara .
Social Plugin