Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Rais Mstaafu wa Kenya, Mhe. Emilio Mwai Kibaki, kilichotokea tarehe 21 Aprili, 2022 jijini Nairobi.
Maombolezo hayo yataanza tarehe 29 Aprili, 2022 hadi tarehe 30 Aprili, 2022.
Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zetu pia.
Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa nchi jirani ya Kenya katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo.
Social Plugin