****************
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba Sc imeendelea kutka dozi mechi za kimataifa nara baada ya leo kuichapa klabu ya Orlando Pirates Fc bao 1-0 katika dimba la Benjamini Mkapa.
Bao hilo liliwekwa kimyani na beki kisiki Shomari Kapombe ambaye alipiga penati nzuri ambayo ikazama moja kwa moja wavuni.
Simba Sc imeendelea kuutendea haki uwanja wake wa nyumbani kwani imekuwa ikifanya vizuri kwenye michezo mingi akiwa nyumbani.
Simba Sc itawafuata Orlando Pirates Fc katika mechi ya marudiano ambayo itapigwa Johannsburg nchini Afrika Kusini, mechi itakayopigwa Aprili 24.
Social Plugin