MWENYEKITI wa Michezo wa klabu ya Michezo ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), David Mwamakula (kulia) akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya soka ya wakala huo, wakati wa mapumziko, ilipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mahakama Sports, Katika Uwanja wa Chuo cha Sheria, Sinza, ili kujiandaa na michuano ya Mei Mosi itakayofanyika Dodoma mwaka huu.
MWENYEKITI wa Michezo Klabu ya Michezo ya Wakala ya Barabara Tanzania(TANROADS), David Mwamakula amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mashindano ya Mei Mosi, mwaka huu.
David alitoa kauli hiyo wakati ya mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya mpira wa miguu ya Mahakama ya iliyofanyika Ijumaa, Aprili Mosi ikiwa ni maandalizi ya michuano ya Mei Mosi, itakayofanyika Dodoma hivi karibuni. Katika mchezo huo timu zote zilitoka sare ya bila kufungana.
Katika michuano hiyo, TANROADS itashiriki katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete(Netball), kuvuta kamba ambapo kuna wanawake na wanaume, riadha wanawake na wanaume, mbio za baiskeli wanawake na wanaume, mchezo ya jadi ikiwemo bao, karata.
Alisema wamejipanga vyema na ndio maana wameanza mazoezi mapema ili kuleta ushindi kwa TANROADS kutokana na kuwa na wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa katika kila eneo uwanjani.
''Tuko vizuri katika kazi na ndio maana tunatekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa. Hivyo katika soka ushindi ni kawaida tu...Tunazitahadharisha timu zote tutakazokutana nazo wajiandae'' alisema.
Hivyo, alisema wamedhamiria kufanya vizuri katika michuano ya Mei Mosi mwaka huu katika kila mchezo kwa kuwa wamekuwa wakiendelea na mazoezi makubwa ili kuhakikisha wanafanya vyema katika michuano hiyo.
Social Plugin