Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bi.Bahati Geuzye wakifanya mazoezi ya viungo katika Tamasha la Michezo Maalumu kwa watumishi hao lililofanyika leo Aprili 02, 2022 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bi.Bahati Geuzye wakishindana kuvuta kamba katika Tamasha la Michezo Maalumu kwa watumishi hao lililofanyika leo Aprili 02, 2022 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakiwa kwenye mchezo wa kukimbiza kuku katika Tamasha la Michezo Maalumu kwa watumishi hao lililofanyika leo Aprili 02, 2022 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam. Washindi wa shindano la kukimbiza kuku katika Tamasha la Michezo Maalumu kwa watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) lililofanyika leo Aprili 02, 2022 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bi.Bahati Geuzye wakipata picha ya pamoja katika Tamasha la Michezo Maalumu kwa watumishi hao lililofanyika leo Aprili 02, 2022 kwenye viwanja vya michezo vya Chuo cha Ardhi Jijini Dar es Salaam.
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
TAMASHA la Michezo maalumu kwaajili ya watumishi wa Mamlaka ya elimu Tanzania ambalo wanalifanya mara moja kwa mwaka sera ya Ukimwi na magoonjwa yasiyoambukizwa.
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) limeandaa Tamasha la Michezo Maalumu kwa watumishi ili kuweza kujiimarisha kimwili na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuunga sera ya Ukimiwi na magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza katika tamasha hilo leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu TEA, Bi.Bahati Geuzye amesema kupitia tamasha hilo yatawahimirisha katika fikra zao na kuwaweka kwenye hari nzuri ya kimwili.
"Tunahitaji kuwapa wafanyakazi muda wa kufanya mazoezi angalau mara moja kwa mwaka kwani mazoezi haya ni muhimu kuanzia kimwili na kiakili hasa katika kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kazini". Amesema Bi.Geuzye.
Aidha Bi.Geuzye amesema pamoja na kula vizuri mlo unaofaa lakini pia wanatakiwa kufanya mazoezi ili mwili uweze kuwa katika hali nzuri na kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali.
Kwa upande wa mmoja wa waatumishi wa TEA waliojiunga kufanya mazoezi leo Bi.Avemaria Kigosi amesema kupitia programu hiyo inawasaidia katika kujikinga na magonjwa mbalimbali na inawasaidia kujenga mahusiano mazuri kwa wafanyakazi na kutimiza majukumu yao kwa uhakika.