Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Lyabwene Mutahabwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo, Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Lyabwene Mutahabwa akifungua mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)leo Aprili 8,2022 wilayani BagamoyoMkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt.Aneth Komba akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani BagamoyoKatibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt. Charles E. Msonde akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo.Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt Siston Masanja akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo
Mmoja wa walimuwa masomo ya Book keeping na Commerce akiuliza swali ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani BagamoyoBaadhi ya walimu wa Book keeping na Commerce wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Lyabwene Mutahabwa akipata picha ya pamoja na walimu katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*******************
NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO
WANANCHI na hasa vijana wanahitaji kufanya shughuli za biashara ili waweze kujitegemea kwa kujiajiri na pia kutengeneza fursa za ajira hivyo basi kuna umuhimu mkubwa kujikita katika masomo ya book keeping na commerce ili suala hilo lieze kutimia.
Ameyasema hayo leo Aprili 8,2022 Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Lyabwene Mutahabwa wakati akifungua mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Wilayani Bagamoyo.
Amesema, taifa linahitaji watu wenye maarifa, ujuzi, stadi na uelekeo wa masomo ya biashara ili kuweza kufanya biashara yenye tija kubwa kwa mtu binafsi, jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yatasaidia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kuboresha elimu kwa kutoa wahitimu wenye maarifa, stadi, na mwelekeo utakaotokana na ujifunzaji wa masomo hayo yenye tija kubwa katika maisha yao ya kila siku.
Pamoja na hayo amewaasa walimu watakaopatiwa mafunzo hayo kuyazingatia na kuyafanyia kazi katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika maeneo yao ya kazi, ili hatimaye waweze kuboresha elimu nchini.
"Ufanisi wa utekelezaji utakaotokana na mafunzo haya utaliwezesha taifa kufikia lengo la uboreshaji wa elimu unaoendana na matakwa ya kupata nguvu kazi kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa viwanda". Amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt.Aneth Komba amesema kupitia mafunzo hayo, yatawajengea walimu uwezo wa kufundisha masomo hayo ya michepuo kwa ufanisi mkubwa zaidi na kuleta tija katika ufundishaji na ujifunzaji, hatimaye kuinua kiwango cha ubora wa elimu na ufaulu wa wanafunzi katika masomo hayo.
Dkt.Komba amesema mafunzo hayo yatatolewa katika makundi matatu yatakayohusisha jumla ya walimu 980 kutoka shule za sekondari za serikali na zisizo ambapo Kundi la kwanza ni la Walimu 490 wa masomo ya Commerce na Book-Keeping.
"Walimu hawa watahudhuria mafunzo haya katika kituo hiki cha ADEM-Bagamoyo kwa muda wa siku sita (6) kuanzia tarehe 8-13/4/2022. Wakati kundi la pili litakuwa la Walimu 90 wa Masomo ya Ufundi watakaopata mafunzo haya katika shule ya sekondari ya Tanga Ufundi kwa muda wa siku 6 kuanzia tarehe 20-25/04/2022". Amesema Dkt.Komba.
Vilevile amesema Kundi la tatu litakuwa la walimu 400 wa masomo ya Home Economics na Agriculture watakaohudhuria mafunzo haya katika Chuo cha ualimu Morogoro kwa muda wa siku sita (6) kuanzia tarehe 1/05/2022 hadi 06/05/2022.