Dkt. MAGEMBE AFUNGUA CHA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UKIMWI KWA WARATIBU NA WAHASIBU WA AFYA

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe akisisitiza jambo wakati akifungua Kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kwa waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kwa waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Mratibu wa UKIMWI kutoka OR-TAMISEMI Dkt.Neema Mlole akizungumza katika Kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kwa waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Afisa Msimamizi wa fedha wa mradi wa Global Fund OR-TAMISEMI Bw.Emmanuel Mwaisabila akiwa katika Kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kwa waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mradi wa Global Fund OR-TAMISEMI Dkt.Mwanahamisi Hassan akifuatilia Kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kwa waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw..Ayoub Kibao akifuatilia Kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kwa waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe akipata picha ya pamoja na baadhi ya Waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri katika kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe akipata picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka Wizara ya Afya katika Kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kwa waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na Halmashauri wakiwa katika kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI kilichofanyika leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

Waratibu wa UKIMWI na wahasibu wa Afya wa Mikoa na halmashauri nchini wamtakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia uwekwaji wa takwimu za wagonjwa, dawa,fedha pamoja na rasilimali zote za miradi ili kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za UKIMWI leo Aprili 11,2022 Jijini Dar es Salaam,Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe amesema watawapima utendaji wao wa kazi kwa kuzingatia ufanisi wao katika kusimamizi miradi hiyo ikiwemo hoja za ukaguzi.

"Kama wewe ni mhasibu au mratibu unaonekana unasababisha hoja za ukaguzi kila siku na zikisababisha huzijibu kwa wakati, wewe haufai kuwa kiongozi kwenye nafasi yako kwahiyo tutakutoa kwa vigezo hiyo ili tuweke mtu ambaye atazingatia kanuni, taratibu na sheria za utumishi katika utendaji wa Umma.

Aidha Dkt.Magembe amewasisitizia umuhimu wa kufuatilia wagonjwa kwa kuhakikisha kwamba wanapata huduma bora kwa wakati na kwa vigezo vimewekwa kitaifa na vilevile kimataifa.

Amewasisitizia pia suala zima la kusikiliza au kupata mrejesho kutoka kwa wananchi ambao wamewahudumia ili waweze kuwaambia uzuri au mapungufu ya huduma zao ambapo mara nyingi wanatoa huduma wakiwa wamejifungia

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Global Fund OR-TAMISEMI Dkt.Mwanahamisi Hassan amesema wanafanya tathimini ya utekelezaji kuangalia ni nini ambacho wametekeleza mpaka sasa katika mradi na changamoto ziko wapi ili waweze kuziondoa changamoto kwasababu mradi unategemeea na matumizi ya fedha mbazo zimepangwa.

"Tunatathimi, tunaangalia utekelezaji wa mwaka mzima, changamoto ziko wapi, tumefanyaje kazi, kama tumefanya vizuri tunapongezana lakini changamto ndogondogo hazikosekani ndo maana tuko hapa kujadili na waratibu wote wa halmashauri zote 184 pamoja na wahasibu kwasababu hzi kazi lazima turipoti". Amesema Dkt.Mwanahamisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post