RC MBUGE: WATAKAO PANDISHA BEI ZA BIDHAA SOKONI WATANYANG'ANYWA LESENI ZA BIASHARA


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge akiwa na kamati ya ulinzi na usalama.
Baadhi ya viongozi wa idara mbalimbali walio hudhulia maadhimisho ya Muungano.

****************

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amepiga marufuku kwa wafanyabiashara kupandisha bei za bidhaa sokoni.

Ameyasema hayo katika maadhimisho ya Muungano yaliyofanyika katika ukumbi wa Bukoba Sekondari yaliyo hudhuliwa na viongozi mbalimbali.

Amesema kumekuwepo na utamaduni wa Wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya Mkoa jambo ambalo halihusiani kabisa na vita vya Urusi na Ukrene ambayo ndiyo imekuwa ni kisingizio.

Amesema kuwa kwa mfanyabiashara yeyote atakaye kiuka agizo na kuendelea kupandisha bei za bidhaa atanyang'anywa leseni ya biashara.

Sambamba na hayo mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kushiriki kikamilifu zoezi la sensa na kutoa ushirikiano kwa maafisa wa zoezi hilo kwani linafaida kwa jamii husika, kwamba baada ya zoezi hilo itatengwa bajeti ya maendeleo kulingana na idadi yao hivyo wote wanatakiwa kuhakikisha wamehesabiwa kikamilifu.

Pia amewashukuru wananchi wa Kagera kutokuwa kikwazo katika zoezi linalo endelea la Post code na badala yake wamekuwa wakitoa ushirikiano.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post