Mshindi wa Sh Milioni 10 Muhidin Salumu Hassani, akifurahia baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya CRDB, Tawi la Palm Beach, jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Sh Milioni 10 Muhidin Salumu Hassani, akifurahia baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya CRDB, Tawi la Palm Beach, jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano wa benki ya CRDB, Tawi la Palm Beach jijini Dar es Salaam, Theresia Mwamunyange kulia, akimkabidhi fedha zake mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko, Muhidin Salumu Hassan, aliyeshinda sh Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa ya Mei Mosi iliyofanyika Jumapili iliyopita. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Afisa Uhusiano wa benki ya CRDB, Tawi la Palm Beach jijini Dar es Salaam, Theresia Mwamunyange kulia, akiwa na mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko, Muhidin Salumu Hassan, aliyeshinda sh Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa ya Mei Mosi iliyofanyika Jumapili iliyopita.
**
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mkazi wa Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, Muhidin Salumu Hasssan, amefanikiwa kukabidhiwa fedha zake sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya Biko iliyochezeshwa Jumapili iliyopita kwenye droo ya Mei Mosi, jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia ushindi wake mbele ya Balozi wa Biko Kajala Masanja na Afisa Uhusiano wa bank ya CRDB, Tawi la Palm Beach, Theresia Mwamunyange, Muhidin alisema fedha hizo amezipata wakati anakabiliwa na ukata, pamoja na ndoto nyingi za kujikwamua kiuchumi.
Muhidin aliishukuru Biko kwa kumkabidhi fedha zake mapema sambamba na kuwataka Watanzania wote wanaocheza biko kuongeza bidii ili nao wajiweke kwenye kundi zuri la kushinda mamilioni kwa kwa kucheza live www.biko.co.tz au kwa namba ya Kampuni 505050 na 2456 namba ya kumbukumbu.
Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wamekuwa kuanzia sh 2500 hadi Milioni 5 papo kwa hapo pamoja na droo kubwa za kila Jumapili, huku ushindi wa papo kwa hapo ukiwa ni hadi Sh Milioni 5.