Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MILIONI 10 ZAENDA TABATA KWA AZIZA SELEMANI


Mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Aziza Selemani akionyesha shangwe la aina yake baada ya kuibuka mshindi wa droo kubwa ya bahati nasibu ya biko na kuvuna Sh Milioni 10 za mchezo huo wa kubahatisha. Makabidhiano hayo yalifanyika bank ya CRDB, Tawi la Primier, lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu.
Mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam, Aziza Selemani katikati akiwa ni mwenye tabasamu pana wakati anakabidhiwa fedha zake Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko, droo iliyofanyika Jumapili iliyopita. Kushoto kwake ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja huku kulia akishuhudiwa na Jackline Mgeni, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa bank ya CRDB, Tawi la Primier, lililopo Palm Beach, jijini Dar es salaam
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa bank ya CRDB, Tawi la Primier, lililoo Palm Beach jijini Dar es Salaam, Jackiline Mgeni kulia akishiriki makabidhiano ya Sh Milioni 10 kwa mshindi wa bahati nasibu ya Biko, Aziza Selemani katikati. Mwingine kushoto ni Balozi wa Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja. 
Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kushoto akimkabidhi fedha zake mshindi wa Sh Milioni 10 za biko, Aziza Selemani, alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa iliyochezeshwa Jumapili iliyopita. Makabidhiano hayo yalifanyika bank ya CRDB, Tawi la Primier, lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam.

***


Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SHILINGI milioni 10 za bahati nasibu ya biko zimeenda kwa Aziza Selemani, mjasiriamali mdogo mwenye maskani yake Tabata jijini Dar es Salaam, anayejishughulisha na biashhara ya usambazaji wa mayai, huku akisema kuwa fedha hizo zimetokana na juhudi zake za kucheza mara kwa mara.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Aziza alisema amekuwa akicheza biko kwa matumaini ya siku moja kuja kuibuka mshindi, jambo ambalo limefanikiwa, akisema huwa anacheza kwa kuingia www.biko.co.tz na wakati mwingine kutumia mfumo wa namba ya kampuni 505050 unaoenda sambamba kwa kuweka 2456 kama kumbukumbu namba.


Alisema Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wamekuwa kuanzia sh 2500 hadi Milioni 5 papo kwa hapo pamoja na droo kubwa za kila Jumapili.


"Namshukuru Mungu leo kukabidhiwa fedha zangu nilizoshinda kutoka kwenye mchezo huu ambao kila mtu anaweza kushinda. Nawashauri Watanzania wenzangu nao wacheze ili waweze kutangazwa mshindi kama ilivyokuwa kwangu,"alisema Aziza.


Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com