Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo akielezea kuhusu Vitisho vya Kidijitali kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo amesema Dijitali imetoa fursa kwa Maudhui ambayo huenda yasingekuwa rahisi kuruhusiwa na Mhariri au Chombo cha Habari.
Ameeleza hayo Mei 01, 2022 katika Mjadala kuhusu Vitisho vya Kidijitali kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari uliofanyika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Akizungumza kwenye Mjadala huo amesema kuna uoga wa mabadiliko kwenye safari ya Dijitali "Najua kuna uoga wa mabadiliko, na changamoto kubwa anayoona ni digitali imekuwa ikidhibitiwa kisiasa".
Vilevile akizungumza Mjadala mwingine kuhusu Mikakati na Mbinu za kupambana na ufuatiliaji wa kidijitali, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums amesema katika dunia ambayo Nchi haiweki Sheria ya Faragha, utu wa watu wake unaweza kuwa matatani.
Amesisitiza Utu katika ulimwengu wa kidijiti ni wa kupigania kwa nguvu zote, akisema JamiiForums kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali inaendesha mafunzo ya usalama wa kidijiti.
Amesema "JamiiForums ni rafiki mkubwa wa Wanahabari na tunaahidi kufanya mafunzo haya kwa Waandishi wa Habari".
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mwaka 2022 yanayobeba Kaulimbiu isemayo, "Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti" yatahusisha Wadau wa Tasnia Habari kutoka ndani na Nje ya Nchi.
Kilele chake ni Mei 03, 2022 na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Social Plugin