Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MISA - TAN YAIPONGEZA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA UPATIKANAJI WA INTANETI, MABADILIKO CHANYA YA UKUAJI WA SEKTA YA HABARI


Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari (kushoto) akiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari (kushoto) akiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa Internet (Intaneti) nchini huku ikiziomba serikali za Afrika ziweke mazingira wezeshi kwa wazalishaji wa maudhui wa ndani ya nchi kunufaika na wanachozalisha kutoka kwa wanaotumia maudhui yao ambao ni Google, Meta,Netflix, Sporty na wengine ambao ni wakubwa kwenye eneo hilo.


Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania MISA – TAN, Bi. Salome Kitomari wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .

Kitomari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA KANDA, na mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe linalomikiwa na Kampuni ya The Guardian Limited amesema MISA-TANZANIA inampongeza Rais Samia Suluhu kwa kazi nzuri anayoifanya ya kututumikia Watanzania huku ikiahidi ushirikiano katika ujenzi wa taifa Tanzania.


“Tangu umeingia madarakani Machi,mwaka 2021,tumeona mabadiliko chanya ya ukuaji wa sekta ya habari nchini,tunaona uhuru wa kujieleza,upatikanaji wa taarifa na vyombo vya habari unazidi kuongezeka siku hadi siku na tumeshuhudia vyombo vya habari vilivyokuwa kifungoni vimefuguliwa.

Tunatarajia serikali yako itaendelea kusaidia ukuaji wa sekta ya habari,ikiwamo kuendelea kujenga mazingira mazuri na wezeshi kwa wafanyabiashara au waliowekeza kwenye vyombo vya habari ili waweze kutoa maslahi mazuri kwa wanahabari”,amesema Kitomari.

“Tunakushukuru wewe na serikali yako kwa kuona changamoto za sheria zinazosimamia taaluma yetu na kuanza kuchukua hatua mbalimbali,ikiwamo mabadiliko ya kanuni ambayo yalikwaza kazi yetu,lakini jitihada zilizopo sasa za kutushirikisha wadau wote wa habari kupitia sheria za habari, ili kuondoa vifungu vinavyokwaza pande zote ni hatua za kutia moyo.Tunaomba wadau wote tushirikishwe kikamilifu”,ameongeza Kitomari.

Amefafanua kuwa licha ya mafanikio mengi kwenye sekta ya habari, bado kuna nitaje changamoto chache zilizopo ambazo zinahitaji ushiriki wa wadau wote na watanzania kuzitatua ikiwemo baadhi ya sheria kuwa kitanzi kwa vyombo vya habari “Tunashukuru hili limeanza kufanyiwa kazi,tunatarajia mabadiliko ya sheria”.


Kitomari amezitaja changamoto zingine kuwa ni hali duni ya maisha kwa waandishi wa habari kutokana na vyombo vingi kushindwa kulipa mishahara kwa wakati au kutolipa kabisa,kwa sababu mbalimbali ikiwamo hali ngumu ya biashara pamoja na Ushindani usio sawa kwenye matangazo kwa vyombo vya masafa ya ndani na vile vya nje,unaochangia kupunguza mapato kwa vyombo vya ndani ambavyo vimeajiri wengi.

Amebainisha kuwa kukosekana utaratibu mzuri utaongeza changamoto ya ajira na kulipa wanahabari,pia ipo changamoto ya kodi ambayo ni kilio cha wamiliki wa vyombo vya habari.

“Changamoto nyingine ni ukuaji wa tekonolojia ulioleta ongezeko la vyombo vya habari mtandaoni ambavyo vingi maudhui yake haifuati matakwa ya taaluma ya uandishi wa habari na Wananchi kutumia uhuru wao wa kujieleza mitandaoni (Citizen journalism)ambao wakati mwingine unafananishwa na taaluma ya habari kiasi cha wengi kushindwa kutofautisha na kujiita wanataaluma licha ya kutokuwa na vigezo”,ameeleza Kitomari.

“Lakini baadhi wananchi kutumia maudhui hiyo (inayorushwa na wananchi) kuhukumu waandishi wa habari wote kuwa hawajui matakwa ya taaluma yao”,ameongeza Kitomari.


KUHUSU MISA TANZANIA

MISA TANZANIA ni sehemu ya Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) yenye makao makuu yake nchini Zimbabwe ikiwa na matawi katika nchi tisa za SADC ambazo ni Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana, Angola, Msumbiji, Lesotho,Afrika Kusini na Eswatn. Ilianzishwa mwaka 1991 kwa azimio la Windhoek, Namibia ambalo liliitambua siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kama siku ya uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni miaka 31 sasa, na MISA ilipewa jukumu la kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika.

Kwa Tanzania aliyeshiriki kuanzisha Misa Tanzania ni Mzee Ndimara Tigambagwe.

Malengo ya kuwepo kwa MISA ni kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa unakuwepo,ukuaji wa vyombo vya habari imara vinavyowajibika na mazingira mazuri ya uandishi wa habari katika nchi wanachama kwa maendeleo na ustawi wa nchi zetu.

Pia kuhakikisha umma unapata taarifa,na ndiyo maana kila Septemba katika Right to know Day MISA Tanzania hutoa kufuli kwa taasisi za umma ambao zilifungia taarifa na funguo kwa zilizofungulia taarifa,hii hufanyika kwa utafiti kwa kupeleka maombi ya taarifa kama mwananchi wa kawaida kwenye ofisi husika, kuwaandikia barua pepe zilizowekwa hadharani kwenye tovuti ,kuwapigia simu kwa namba walizoweka kwenye tovuti, lengo ni kuona namna gani mwananchi wa kawaida kabisa anapata taarifa za maendeleo kwa urahisi na kuongeza uwajibikaji kwenye kutoa taarifa kwa taasisi za umma.

MISA-TANZANIA ni taasisi ya wanachama mmoja mmoja na taasisi za kihabari,ina wanachama zaidi ya 250 waliosambaa kwenye kila mkoa nchini,inafanya uraghbishi, inatoa mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wanahabari kwenye kuzijua sheria zinazosimamia taaluma na sheria za nchi,maadili ya uandishi wa habari na habari za jinsi katika kuondoa mfumo dume na kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye maudhui na nafasi za uongozi.


Pia MISA-TANZANIA imetoa msaada wa kisheria kwa baadhi wanahabari waliopata changamoto mbalimbali wakiwa kazini.

MISA ilikuwa mwangalizi wa kimataifa kwenye uchaguzi mkuu wa Zambia,Agosti mwaka 2021.

Imekutana na Jumuiya za Kikanda na serikali za nchi mbalimbali inapotokea kuna sheria zinazokwaza kazi za uandishi wa habari na hivi karibuni MISA TANZANIA ilikutana na serikali ya Botswana ambayo ilipokea hoja za Misa Tanzania na kuahidi kurudisha muswada kwa wadau kabla ya kupeleka bungeni.

Soma pia :

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com