**
Na Rahma Idrisa Haji - Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Othman Masoud Othman anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya uhuru wa habari duniani kwa upande wa Zanzibar Jumapili Mei 22,2022.
Akitoa taarifa ya madhimisho hayo mbele ya vyombo vya habari katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( SUZA )Idara ya mawasiliano na mafunzo ya habari kilichopo kilimani Mkoa wa Mjini Magharibi Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya siku ya uhuru wa habari duniani kwa upande wa Zanzibar Faroq Qareem amesema kuwa Madhimisho hayo yanategemewa kufanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil kuanzia saa 2:30 Asubuhi Mei 22,2022.
Amesema kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anategemewa
kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ambapo
waandishi wa habari mbalimbali watahudhuria ikiwemo wadau wa Habari kutoka
katika asasi za Kiraia kutoka Zanzibar.
"Maadhimisho haya ya mwaka huu yataambatana na uwasilishwaji wa mada mbili ambazo ni hali
ya uandishi wa kwa Zanzibar ikiwemo matumizi ya Teknolojia na mapungufu ya
sheria ya habari, hata hivyo kutakuwa na ushuhuda wa waandishi wa habari katika
mafanikio na changamoto zao wakati wa kutekeleza majukumu yao",amesema
Qareem amesema kuwa Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba ujumbe
muhimu ambao ni UANDISHI WA HABARI NA CHANGAMOTO ZA
KIDIGITI Lakini kwa Upande wa Zanzibar kuna kauli mbiu isemayo UANDISHI
WA HABARI ZANZIBAR MUELEKEO NA CHANGAMOTO.
Akizungumzia kuhusu shindano la Tuzo za umahiri kwa
waandishi wa habari amesema kuwa mara hii tuzo hizo zitafanyika tarehe 28 mwezi
wa 9 mwaka huu ambapo ni kilele cha siku ya kujua duniani (WORLD RIGHT TO KNOW
DAY ) kwa lengo la kuwapa fursa waandishi wengi kuweza kushiriki shindano hilo
.
"Tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari zitakuwa
katika vipengele vifuatavyo
TUZO YA UCHUMI WA BULUU ( DK MWINYI AWARD )
TUZO YA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ( MAALIM SEIF AWARD )
TUZO YA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA ( ZAEKA AWARD )
TUZO YA KULIPA KODI (
ZRB AWARD )
TUZO YA UKIMWI NA AFYA
TUZO YA UWAJIBIKAJI ( SECOND VICE PRESIDENT AWARD )
TUZO YA MAZINGIRA ( FIRST VICE PRESIDENT AWARD )
TUZO YA JINSIA
TUZO YA UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINAADAMU.
Social Plugin