KATIBU Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Bohari
ya Dawa (MSD) kufanikisha upelekaji wa vifaatiba katika Hospitali ya
Wilaya ya Ushetu Mkoani Shinyanga ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Chongolo
ametoa agizo hilo leo Mei 28,2022 wakati wa ziara yake ya kukagua jengo
la Hospitali hiyo ya Wilaya ya Ushetu ikiwe ni muendelezo wa ziara zake
katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Amesema atazungumza na
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu MSD kuchelewesha uletaji wa
vifaatiba hivyo lakini pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia
Mjema kumtafuta mhusika wa Bohari ili aweze kukutana nae.
"
Niagize ndani ya mwezi huu au mwezi ujayo hivyo vifaa viwe vimefika hapa
ili vianze kutoa tiba na huduma kwa wananchi wetu, haiwezekani Rais
wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan anashusha fedha nyingi huku kuja
kutengeneza miundombinu ya Kisasa halafu vifaatiba inakua ni hadhithi,
hili halivumiliki.
Hatupo tayari kuona watu wachache wanakwamisha
juhudi zinazofanywa za kuwahudumia wananchi wetu, CCM tuliahidi kupitia
ilani yetu mwaka 2020 na tunatekeleza," Amesema Chongolo.
Awali
Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani alimueleza Katibu Mkuu Chongolo
kwamba walipokea sh Bilioni 3.2 kwa ajili ya Hospitali hiyo lakini licha
ya majengo baadhi kukamilika bado hawajaletewa vifaatiba na wahudumu
kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Wilaya hiyo.
"Tunaomba Katibu
Mkuu utusaidie kutusemea Hospitali imeshakamilika ila vifaatiba na
wahudumu ndo changamoto, inatulazimu kuwapeleka wagonjwa zaidi ya km 40
hadi Kahama.
Majengo tayari tunachoomba utusaidie vifaatiba
vifike pamoja na wahudumu wa Afya ili wananchi hawa wa Ushetu wasiwe
wanatembea umbali mrefu kufuata matibabu," Amesema Cherehani.
Ujenzi
wa Hospitali hiyo umetekelezwa kwa awamu tatu na ulianza January 2019
ambapo Serikali imepeleka fedha jumla ya Sh Bilioni 3.2 kwa ajili ya
kukamilisha.
Picha
mbalimbali zikionesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel
Chongolo akikagua ujenzi wa jengo la utawala katika hospitali hiyo.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG
Muonekano wa jengo la Utawala wa hospitali hiyo ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelekezo
kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya. Wilaya ya Ushetu mkoani
Shinyanga,Dk. Nicodemus Senguo wakati alipokagua akikagua ujenzi wa
majengo mapya ya hospitali ya wilaya hiyo leo Mei 28,2022.
Moja ya jengo la hospitali hiyo likiendelea kujengwa
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo kimsikiliza Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM,Kanali Mstaafu Lubinga Ngemela
wakati akitoa maoni yake katika ukaguzi wa ujenzi wa hospitali hiyo.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akitoa maelekezo Kwa
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga, Dk
Nicodemus Senguo wakati alipokagua ujenzi wa majengo mapya ya hospitali
ya wilaya hiyo inayojengwa katika Kijiji Cha Mtonga kata ya Nyamilangano
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akzungumza jambo na
msaidizi wake Bw. Saleh Mhando mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi
wa jengo la utawala katika hospitali hiyo.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipitia Daftari la
wanachama la shina namba 6, Tawi la Mitonga, Ushetu kulia ni Mwenyekiti
wa shina hilo Ndugu Masanja Bundara ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake
mkoani Shinyanga,kulia ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM,Kanali Mstaafu Lubinga Ngemela
Wannachi
wa kijiji cha Mtonga kata ya Nyamlingano wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wakaati akizungumza nao mara
baada ya kukagua ujenzi huo wa Hospitali ya Wilaya ya Ushetu mkoano
Shinyanga.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Kanali mstaafu
Ngemela Lubinga akifafanua baadhi ya mambo katika kikao hicho.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na
wananchi wa Kijiji Cha Mitonga baada ya kukagua ujenzi wa jengo la
utawala katika hospitali hiyo
Mbunge wa jimbo la Ushetu Mhe.Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye mkutano huo wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Daniel Chongolo.
Social Plugin