Suleiman Mangara Kamimu Mwenyekiti wa Taaisis ya Jicho la Mama Samia akizungumza nawaandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayafanya ili kuwaletea maendeleo watanzania kutoka kushoto ni Bahati Ally Kaimu Katibu Mkuu Jicho la mama Samia na Shaweji Mkumbula Katibu Mkuu Jicho la Mama Samia katika mkutano huo umeofanyika kwenye hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam.
Shaweji Mkumbula Katibu Mkuu Jicho la Mama Samia akisoma tamko la taasisi hiyo leo kuunga mkono shughuli za Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye hoteli ya Nefaland Manzese jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Felix Makua Mratibu Msaidizi wa Taaisis ya Jicho la Mama Samia na Bahati Ally Kaimu Katibu Mkuu Jicho la mama Samia
Mkutano ukiendelea.
..........................................
Rais wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ameingia katika Historia ya kuwa Mwanamke wa Kwanza hapa Nchini Tanzania kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kwa kudra za Mwenyezi Mungu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo halikuwa limetegemewa na Watanzania walio wengi.
Rais Samia amejipambanua kwa mambo mengi anayoendelea kuyatekeleza hapa nchini katika miradi ya Kimkakati kama Miundo Mbinu, Reli ya Kisasa (SGR) Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere na Daraja la Kigongo Busisi, ikiwa ni pamoja na mradi mkubwa wa anwani za Makazi pamoja na zoezi la Sensa ambalo linaenda kutekelezwa Mwezi Agosti mwaka huu ili kama nchi kujiwekea mipango ya baadaye namna bora ya kuwahudumia wananchi.
Ni jambo kubwa kuyasemea mambo makubwa na mazuri ambayo yanayofanywa na Rais chini ya serikali ya awamu ya 6 tuendelee kuyaainisha na kueleza kuwa anafanya Vizuri katika haya na haya yanahitaji maboresho katika jambo hili na lile, kwa yale yenye Changamoto tutaendelea kumueleza Changamoto na kupendekeza utaratibu bora na wenye tija katika Utatuzi wa Changamoto hizo
Hayo yamesemwa na Suleiman Mangara Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi ya Jicho la Mama Samia ambayo moja ya majukumu yake ni Kufanya Utafiti na kufuatilia mambo yanayofanywa na rais katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi.
Mangara amesema watanzania wote tunafahamu kuwa moja ya Chanzo kikubwa kinachoingiza fedha za Kigeni ni UTALII, Nchi nyingi Duniani ambazo zimefanikiwa kuwa na Vivutio mbalimbali huwa zinafanya jitihada kubwa kutangaza vivutio vyake ili kuvutia watalii kutembelea nchi zao na hivyo kuingiza fedha nyingi za Kigeni.
Jambo lingine ni kuvutia uwekezaji kutokana na fursa za vivutio vilivyomo katika Nchi ambapo wawekezaji wanaweza kuona umuhimu wa kuja Kuwekeza.
Amempongeza Sana Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa Kuitangaza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar na Vivutio vyake kupitia Filamu ya Tanzania Royal Tour iliyozinduliwa hivi karibuni huko Marekani na baadae Tanzania Arusha, Dar-es-Salaam na Zanzibar
"Tukio la Rais kuamua kushiriki katika Filamu ya Kuitangaza Tanzania akiwa kama Muigizaji Mkuu ulikuwa ni UAMUZI MKUBWA unaopaswa kuungwa Mkono na Watanzania walio wengi na kiukweli umevutia watu wengi jambo ambalo linaifanya Tanzania kujulikana zaidi duniani,". Amesema Suleiman Mangara.
Uzinduzi huo uliofanyika kwa mara ya Kwanza nchin Taifa la Marekani, na uzinduzi uliofanyika Nchini Marekani katika miji ya New York na Los Angels ambayo ina watu wengi mashuhuri na wafanyabiashara wakubwa ilikuwa ni fursa nzuri kwa nchi kujulikana na kuvutia watalii na wawekezaji pamoja na wafanyabiashara mbalimbali.
Kupitia fursa ya uzinduzi tu mikataba ya uwekezaji iliyosainiwa inafikia shilingi za Kitanzania Triliion 11.7. ambayo itaanza kuja kuwekezwa Tanzania, huu ni ushindi Mkubwa kuwa Rais wetu anazidi kuiimarisha nchi kiuchumi. .
Akizungumza hali ya siasa nchini Mangara amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kurekebisha kasoro katika suala zima la Demokrasia ya Mfumo wa Vyama vingi ambalo lilikuwa linalalamikiwa sana na wadau wa Demokrasia wa Ndani na Nje ya Nchi.
Uamuzi wa Rais Samia kuruhusu na serikali kugharamia Mkutano wa Wadau wa Demokrasia uliofanyika Dodoma katikati ya Mwezi Desemba 2021. ulioandaliwa na Kituo cha Deokrasia Nchini Tanzania Centre for Democracy (TCD) ulikuwa ni sahihi na wenye busara na hekima kubwa.
Mkutano ule ambao uliohudhuriwa na wadau wa Demokrasia lakini pia Mabalozi wa Nchi mbalimbali duniani ulijadili kwa uhuru changamoto za Deokrasia ikiwamo Mkwamo wa Katiba lakini pia kuazimia mapendekezo yote yataenda kwenye Kikosi kazi kilichoundwa na Rais ili kutatua changamoto hizo za kisiasa.
Kama Taasisi tunampongeza Rais Samia kwa uamuzi wake na utashi wake wa kisiasa kuamua kurekebisha kasoro zote zinazoonekana kufifisha demokrasia ya Mfumo wa Vyama Vingi Tanzania.
Katika hatua nyingine Bw. Mangara kipekee amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ongezeko la mishahara kwa asilimia 23.3 kwa wafanyakazi jambo ambalo kiukweli linaleta faraja kubwa kwa wafanyakazi ambao walikaa miaka 6 bila ya kupanda madaraja na bila ya ongezeko la Mishahara hii inadhihirisha kwamba mama ni mlezi mzuri kwa watoto wake.
Katika suala zima la kupanda kwa bidhaa taasisi hiyo imetoa ushauri kwa mamlaka zinazomsaidia Rais kuhakikisha zinamshauri kwa dhamira njema na kutambua nia aliyonayo kwa wananchi wake na kumshauri kwa hekima na busara.
"Mamlaka zimulike hadi chini ziangalie wafanyabiashara wanaopandisha Biashara Kiholela na kuwaumiza sana wananchi pia mamlaka zinazodhibiti bei, pamoja na uwepo wa sera ya Soko Huria ni muhimu kukawepo na bei elekezi hadi ngazi za Chini ili kusiwe na mkanganyiko mkubwa wa bei katika soko ambao umekuwa ukiumiza sana wananchi,".Amemaliza Mangara.
Social Plugin