Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya kaskazini Dismas Prosper akikabidhi mfano wa hundi ya milioni 59 kwa mkurugenzi wa maonyesho ya Kill fair ikiwa ni ufadhili wao katika maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 3 Hadi Tano jijini Arusha
Na Rose Jackson,Arusha
WADAU wa utalii kutoka nchi 38 duniani wamethibitisha kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Karibu-Kili Fair yanayotarajiwa kuanza Juni 3 hadi 5 mwaka huu mkoani Arusha.
Akizungumza jijini Arusha, Mkurugenzi wa Kilifair Ltd ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo, Dominic Shoo amesema lengo la maonyesho hayo kutangaza vivutio vilivyopo nchini.
Amesema tayari nchi hizo zimeshathibitisha ushiriki wa maonyesho ya Kili fair ambayo kwa asilimia kubwa yanalenga kutangaza utalii .
"Royal Tour aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan imetusaidia kuitangaza nchi,hivyo Dunia inafahamu Tanzania,imetupa urahisi mkubwa sanaaa wakufanya Kili - fair",anasema Shoo
Amesema onyesho hilo litakuwa la kipekee, baada ya Dunia kukumbwa na janga la Covid-19 na kutakuwa na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.
"Katika maonyesho haya pia tunatarajia washiriki 380 kutoka nchi hizo na wengine kutoka nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao wametuomba tutangaze vivutio vilivyopo katika nchi hizo kama vivutio vya pamoja,"amesema.
Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Kaskazini,Dismas Prosper amesema wao pia ni miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo, wakiamini utalii ni sehemu kubwa ya uchumi Kanda ya Kaskazini.
Amesema pia katika kunyanyua sekta ya utalii pia wamefadhili Sh.milioni 59 katika maonyesho hayo ili yafane na kukidhi haja kwa wageni watakaohudhuria katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini.
"Sisi tumejipanga kuhudumia wageni wetu watakaokuja na waliopo kwa kutoa huduma bora ya kubadilisha fedha kwa kuweka mashine za ATM kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) na tumeboresha na kujenga mahusinao mazuri na wafanyabiashra mbalimbali wa sekta ya utalii,"amesema Prosper.
"Tunahitaji kukuza sekta ya utalii nchini na Benki yetu imejikita katika kuhakikisha inasaidia Kilifear kufanikisha maonyesho ya kimataifa ya kanda hii ya Afrika Mashariki",ameongeza
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi maendeleo ya biashara Beatrice Kessy anasema maonyesho hayo yanasaidia sana kutangaza utalii na fursa zilizopo