TAMKO LA KULAANI MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI, 31, MEI, 2022
Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kimefuatilia kwa karibu matukio ya mauaji yanayoendelea hapa nchini na kinachukua nafasi hii kulaani matukio hayo ya mauaji kwa kuitaka jamii kutojihusisha nayo.
Matukio hayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali , yapo mauaji yaliyofanyika kwa sababu za kimapenzi, tuhuma za wizi na imani za kishirikina.
Visa mkasa hivyo vyote vimesababisha baadhi ya watanzania wenzetu kutolewa uhai wao kinyume na sheria za nchi, ikiwemo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara 14 inayotoa haki ya mtu kuishi.
OJADACT inatoa mapendekezo yafuatayo kwa watanzania, Serikali na Taasisi mbalimbali.
• Serikali ifanye tafiti za kina za kubaini chanzo za mauaji yanayoendelea nchini pamoja na kuwa na mpango wa kuanzisha vituo vya kisaikolojia.
• Wanandoa watarajiwa wawe na muda wa kujuana tabia kwa undani kabla ya kuoana na kufuata mifumo rasmi ya usuluhishi wa matatizo yao
• Jeshi la Polisi litoe elimu sahihi ya matumizi ya silaha kwa wamiliki wa silaha nchini.
• Wazazi wahakikishe wanajihusisha na malezi ya watoto wao na kuepuka kuwaacha watoto wajilee kimaadili.
Edwin Soko
Mwenyekiti .
OJADACT
Soma pia :