Nyumba ya Evaristo Mgimba
MAHAKAMA ya mwanzo Lugarawa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemhukumu Ombeni Ngwa’vi (25) kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba ya Evaristo Mgimba na miaka miwili kwa kuiba debe moja la maharage ambapo vifungo hivyo vitaenda kwa kufuatana na si sambamba.
Akisomewa shitaka hilo Mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu Timoth Mwakisambwe imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Mei 12 mwaka huu majira ya mchana ambapo alivunja nyumba ya Evaristo Mgimba kisha kuiba debe moja la maharage yenye thamani ya shilingi 30,000.
Ombeni Ngwa’vi (25) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba ya Evaristo Mgimba na miaka miwli kwa kuiba debe moja la maharage
Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha sheria namba 294(1)(a), 258(1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019.
Social Plugin