Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Dar es salaam, Paul Makonda amefika katika Ubalozi wa Umoja wa Falme Za Kiarabu nchini na kutia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Hayati Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Paul Makonda amemshukuru Balozi Khalifa Almarzouqi kwa ushirikiano wake katika kukuza mahusiano baina ya Tanzania na Umoja wa Falme Za Kiarabu
Makonda amesema atamkumbuka Hayati Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan kwa mahusiano ya kipekee aliyokuwa nayo na Tanzania katika kudumisha mahusiano ambapo ametoa salaam zake za rambirambi kwa Mtukufu Sheikh Mohamed Bin Zayed Alnahyan na Wananchi Umoja wa Falme Za Kiarabu, pamoja na Kumpa pongezi kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Falme Za Kiarabu na Mtawala wa Abudhabi.
Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Makonda amemshukuru Hayati Sheikh Khalifa kwa ushirikiano aliompa akiwa RC Dar es salaam ikiwemo kusomesha Watoto wa kike 200 kila mwaka, kuleta Madaktari kutoka Dubai na Abudhabi na kufanya upasuaji wa Watoto 78 wasiokuwa na uwezo JKCI, kulipia Bima ya Afya Watoto wote wa DSM na katika mazingira magumu (Yatima na waishio katika Vituo vya kulelea) na kuwezesha kila mwezi la Ramadhani Ifter ya Viongozi wa Misikiti yote kwa mwezi mzima.