Ni seti mbili ya mapacha kama hawa ambao wamewahi kurekodiwa katika historia, lakini hakuna walioishi zaidi ya siku chache.
***
Mapacha tisa wa kipekee waliozaliwa wakati mmoja (wasichana watano na wavulana wanne) wako "katika afya kamilifu" wanaposherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa mara ya kwanza, baba yao ameambia BBC.
"Sasa wanatambaa. Wengine wanaketi na hata kutembea wakijishikilia mahali," alisema Abdelkader Arby, afisa wa jeshi la Mali.
Bado wako katika uangalizi wa kliniki nchini Morocco walikozaliwa.
Alisema mama yao Halima Cissé, 26, pia anaendelea vyema.
"Sio rahisi lakini twamshukuru Mungu. Hata kama inachosha wakati mwingine,unapowaona watoto wote wakiwa na afya njema, [kwenye laini]kutoka kulia kwenda kushoto tunafarijika.Tunasahau kila kitu," aliambia BBC Afrique.
Ndio amerejea nyumbani kutoka Morocco kwa mara ya kwanza ndani ya miezi sita, akiwa na mtoto wake wa kwanza, Souda, mwenye umri wa miaka mitatu.
"Nafurahi sana kujumuika na familia yangu - mke wangu, watoto."
Watakuwa na sherehe ndogo tu ya kuzaliwa wakiwa na wauguzi na watu wachache kutoka kwa jengo lao la ghorofa, Bw Arby alisema.
"Hakuna kilicho bora kuliko mwaka wa kwanza. Tutakumbuka wakati huu mzuri tunaoenda kuupata."
Watoto hao walivunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa watoto wengi zaidi kuzaliwa kwa wakati moja na kuishi.
Kabla ya kujifungua mnamo Mei 4, 2021, Bi Cissé alisafirishwa hadi Morocco na serikali ya Mali kwa uangalizi maalum.
Kuzaa watoto wengi ni hatari na akina mama walio na zaidi ya vijusi wanne kwa wakati mmoja wanashauriwa kuavya mimba hiyo hasa katika nchi ambazo utoaji mimba ni halali.
Pia kuna hatari ya watoto kupata matatizo ya kiafya kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati wao, kama vile sepsi s(kuvimba tishu na viungo) na kupooza kwa ubongo.
Bi Cissé na watoto hao kwa sasa wanaishi katika kile ambacho baba yao alikitaja kama "gorofa yenye tiba" ambayo ni ya wamiliki wa kliniki ya Ain Borja huko Casablanca ambako watoto hao walizaliwa.
"Kuna wauguzi ambao wako hapa, pamoja na mke wangu, ambao husaidia kutunza watoto," Bw Arby alisema.
"Kliniki imewapa menyu ambayo inasema nini cha kuwapa kula wakati wote - usiku na mchana," aliendelea.
Abdelkader Arby, Halima Cissé binti ya Soudawalifurahi san akuwa na familia kubwa hivyo
Watoto hao wasichana watano na wavulana wanne alizaliwa wakiwa na wiki 30 kulingana Waziri wa Afya wa Mali, Fanta Siby. Walikuw ana uzani wa kati ya gramu 500 na kilo moja (1.1lb na 2.2lb), Profesa Youssef Alaoui, mkurugenzi wa matibabu wa kliniki ya Ain Borja clinic aliambia shirika la habari la AFP wakati wa kuzaliwa kwao.
Walizaliwa kupitia njia ya upasuaji.
Wavulana wanaitwa Mohammed VI, Oumar, Elhadji, Bah, nao wasichana wakapewa majina ya Kadidia, Fatouma, Hawa, Adama na Oumou.
Kila mmoja wao ana kitu cha kipekee, baba yao alisema.
"Wate wana tabia tofauti. Wengine ni wapole, huku wengine wakipiga kelele na kulia sana. Wengine wanataka kuokota kila wakati. Wote ni tofauti sana, jambo ambalo ni la kawaida kabisa."
Bw. Arby pia lishukuru serikali ya Mali kwa usaidizi wake.
"Serikali ya Mali ilitayarisha kila kitu kwa ajili ya matunzo na matibabu ya watoto hao tisa na mama yao. Sio rahisi hata kidogo, lakini ni nzuri na ni jambo la kufariji," alisema.
Hawajafika Mali lakini tayari ni maarufu sana nchini humo, baba yao alisema.
"Kila mtu ana shauku kubwa ya kuwaona watoto kwa macho yao - familia zao, marafiki, kijiji chetu, nchi nzima."
Pia ana ujumbe kwa wanandoa wanaojaribu kupata watoto: "Natumai Mungu atabariki kila mtu ambaye bado hajapata watoto - kwamba wanaweza kupata kile tulicho nacho sasa. Ni kitu kizuri, hazina halisi."
Chanzo - BBC Swahili
Social Plugin