Na Hamida Ramadhan Dodoma
MKAZI wa Kijiji Cha Ilangali,Kata ya Manda Tarafa ya Mpwayungu,Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Shabani Chilingo (54) ameuawa na mtoto wake aitwaye Shukrani Chilingo (35) chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
Akizungumzia jijini hapa na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno amesema tukio hilo lilitokea Mei 4 majira ya 3 usiku ambapo mtuhumiwa aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali usoni na sikioni .
Kamanda Otieno amesema mtuhumiwa alimtuhumu baba yake mzazi ambaye ni (Marehemu) kuwa ana mahusiano ya kimapaenzi na mke wake.
” Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili mara baada ya uchunguzi kukamilika,”alisema Kamanda Otieno.
Na kuongeza Kusema”Kujichukulia sheria mkononi ni kosa la jinai jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua za kisheria Watu wote wanaojichukulia sheria mkononi
Katika tukio lingine mtaa wa mailimbili Mnadani jijini hapa Amelia Salamba mwenye Umri wa miezi 10 alikutwa amekufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo ya maji yenye ujazo wa Lita 10 iliyokuwa chooni ambapo mtoto huyo alibaki na msichana wa kazi wakati wazazi waeenda kazini
Social Plugin