Mwili wa Swalha ukisomewa dua nyumbani kwao jijini Mwanza kabla ya maziko.
Mwili wa Swalha ukiingizwa kaburini kwa maziko.
HATIMAYE mwili wa mwanamke Swalha Salum mkazi wa Buswelu wialayani Ilemela jijini Mwanza aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mumewe wa ndoa, umezikwa jijini Mwanza, ambapo majonzi na huzuni vimeendelea kutawala eneo hilo.
Swalha alipigwa risasi Jumamosi Mei 28, 2022 na mumewe, Said Oswayo wakiwa nyumbani kwao katika mtaa wa Mbogamboga, Kata ya Buswelu wilayani humo baada ya kuibuga ugomvi kati yao kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Siku mbili baada ya kutekeleza mauaji hayo huku juhudi za maofisa wa Jeshi la Polisi kumtafuta mtuhumiwa zikiendelea, Jumatatu ya Mei 30, 2022, mwili wa Oswayo ulionekana ukielea kwenye maji ya Ziwa Victoria katika Ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza huku ndugu wakithibitisha kuwa ni mwili wa ndugu yao.
“Hata maandiko ya dini yanatuelekeza kuwa na subra wakati wa matatizo kwa sababu usipofanya hivyo huenda ukasababisha madhara zaidi ya haya yaliyotokea hapa. Pia tumtangulize Mungu katika kila jambo tunalolifanya,” amesema Shehe Salum aliyeondoa mazishi ya mwanamke huyo.
Msanii wa Bongo Fleva, Hamisi Ramadhani (H Baba) ni miongoni mwa waliohudhuria mazishi hayo ambapo amemtaja Swalha kuwa mtu mwenye mchango katika sanaa yake na kusema kwamba mwana urembo huyo alishiriki kumremba katika video zake.
H Baba ameiomba Serikali na Jeshi la Polisi nchini kufanya uchunguzi wa kina na kisaikolojia kabla ya kutoa leseni ya kumiliki silaha kwa mtu yoyote.
“Serikali iangalie upya utaratibu mzuri kabla ya kuwapa watu ruhusa ya kumiliki silaha huenda umakini ungekuwepo haya yasingetokea. Sasa hivi vijana kumiliki silaha imekuwa kawaida,” amesema H Baba akiwa msibani.
Soma pia :
Social Plugin