Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Bw. John Joseph akizungumza
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imebaini mapungufu katika utekelezaji wa mradi ya maendeleo 28 yenye thamani ya zaidi ya bilioni saba Mkoani Kagera.
Akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi uliopo ofisi ya Takukuru Mei 19, 2022, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera John Joseph amesema kuwa katika miradi iliyofanyiwa ufatiliaji ilibainiwa kuwa na mapungufu ikiwemo ya kutumia vifaa vyenye ubora tofauti na ilivyoelekezwa na BOQ.
Amesema kuwa vifaa hivyo walivyobaini mapungufu ni kutumia kioo cha 4mm badala ya 5mm, uwekaji mbaya wa vigae (Tiles), viti kutengenezwa pungufu na ilivyokadiliwa, kutoweka kumbukumbu za utoaji wa vifaa kutoka stoo pamoja na hayo walibaini bei kubwa za baadhi ya vifaa vya umeme na ujenzi kuuzwa bei kubwa kuliko bei ya soko.
Amesemamiradi iliyofautiliwa ni ya ukarabati wa miradi ya maji, ujenzi wa Hospitali, vituo vya Afya, zahanati pamoja na ujenzi wa madarasa chini ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano ya dhidi ya Uviko19.
Bw. Joseph ameongeza kuwa baada ya ufuatiliaji wa miradi hiyo imetolewa Elimu kwa wahusika wa miradi saba ili kuboresha kasoro zilizojitokeza na miradi tisa tayari uchunguzi wa kina unaendelea huku miradi 12 kati ya miradi 28 haikuwa na kasoro na kwamba inaendelea kukamilishwa.
Amewashukuru wana Kagera wote ambao wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa Takukuru pia amewataka kujua kila mwananchi anahitaji kutanguliza maslahi ya Nchi na kuchukua hatua katika kukabiliana na tatizo la rushwa katika Mkoa wa Kagera.
Social Plugin