Mtoto wao amedumu katika ndoa miaka 6 bila mtoto
****
Huko nchini India wazazi wamefungua kesi kwa mtoto wao wa kiume na mkwe wao wakitaka waletewe mjukuu ndani ya mwaka mmoja au walipwe Rupia milioni 50 (Rupia milioni 25 kutoka kwa kila mmoja) sawa na Tsh bilioni 1.5
“Mwanangu amekuwa kwenye ndoa kwa miaka sita lakini bado hawajapata mtoto. Angalau tupate mjukuu wa kukaa naye, maumivu yetu yatavumilika..” maneno ya wazazi hao katika ombi lao lililowasilishwa kwa mahakama ya Haridwar.
Sanjeev na Sadhana Prasad walifungua kesi hiyo katika ya mji wa Haridwar, wakidai mjukuu au walipwe pesa hizo kufidia gharama walizotumia katika harusi yao, gharama walizotumia kumsomesha mtoto wao Marekani mpaka akawa rubani, na gharama walizotumia kuwapeleka fungate nchini Thailand.
Social Plugin